Jiandae na Simu Zenye Kamera ya Mbele Inayojificha Chini ya Kioo

Kampuni za Oppo na Xiaomi za onyesha simu zenye teknolojia hiyo
Jiandae na Simu Zenye Kamera ya Mbele Inayojificha Chini ya Kioo Jiandae na Simu Zenye Kamera ya Mbele Inayojificha Chini ya Kioo

Teknolojia ya simu hasa smartphone inaendelea kusongo mbele kwa kasi sana, ni muda sasa tumeshazoea simu zinazo jikunja na sasa tupo tayari kuona aina mpya ya simu zenye kamera ya mbele ambayo inayo jificha chini ya kioo.

Kupitia akaunti ya Twitter ya Oppo, kampuni hiyo imeonyesha aina mpya ya teknolojia ya kamera ya mbele ambayo imetengezwa chini ya kioo cha simu na hivyo kufanya simu kuonekana na kioo kitupu kisicho na ukingo wowote wa juu wala sehemu yoyote ya kioo iliyo katwa.

Advertisement

Kwenye video fupi hapo juu inaonekana mtu akipiga picha kwa kutumia kamera ya mbele ambayo haionekani moja kwa moja kwenye simu hiyo. Baadae inaonekana mtu huyo akionyesha kuwa kamera hiyo ipo kwa juu kabisa ya kioo cha simu hiyo.

Hata hivyo baada ya muda kidogo, kampuni ya Xiaomi nayo ilitumia akaunti yake ya Twitter kuonyesha teknolojia kama hiyo kwa ukaribu zaidi.

Kwa mujibu wa kampuni ya tovuti ya GSMArena, inasemekana kuwa kampuni ya Xiaomi imegundua teknolojia mpya ya kuweza kufanya kioo cha simu kuwa na uwazi (transparent) ambao kina uwezo wa kuruhusu kamera ya mbele kuweza kuonyesha vizuri bila kuathiri pixel zilizopo kwenye kioo cha simu inapokuwa imewashwa au imezimwa. Kama unavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini, sehemu hiyo ya kamera haionekani kabisa hata kama simu itakuwa imewashwa au imezimwa.

Jiandae na Simu Zenye Kamera ya Mbele Inayojificha Chini ya Kioo

Upande wa kushoto ni simu yenye ukingo wa juu maarufu kama waterdrop notch, na kulia ni simu ambayo inakuja na kamera ya mbele iliyopo chini ya kioo.

Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili ni lini teknolojia hii itaanza kutumika kwenye simu za Xiaomi au Oppo, lakini kutokana na ushahidi huu ni wazi kuwa inawezekana mwishoni mwa mwaka 2020 simu nyingi zikaja na aina hii ya kamera ya mbele.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use