Kabla ya kununua simu iliyotumika ni vyema kuangalia mambo haya ambayo yatakusaidia kununua simu ambayo itakuwa bora na nzima kwa matumizi yako ya baadae. Kumbuka kuwa kuna hatari sana kununua simu iliyotumia, lakini kutokana na sababu mbalimbali unakuta huna namna nyingine hivyo ni muhimu kuzingatia haya kwani yatakusaidia kupata kilicho bora.
- Hakikisha Unakua na Muda wa Kutosha
Katika hatua za kununua simu iliyotumika ni muhimu sana kuwa na muda wa kutosha, kwani ukiwa na muda wa kutosha utapata muda wa kukagua kila kitu kwenye simu unayotaka kununua. Pia ni vizuri kumwambia muuzaji kuwa akupe muda wa kutosha wa kukagua simu anayotaka kukuuzia, kama muuzaji hana muda wa kutosha ni vyema kutafuta siku nyingine ambayo wote mtakua mna muda wa kutosha.
- Usinunue Simu ya Siku Nyingi (Yazamani)
Hakikisha unapo nunua simu iliyotumika basi simu hiyo isiwe ya zamani sana, kwani simu nyingi za zamani sana zinakuwa na matatizo mengi mengine ni madogo madogo kiasi kwamba huwezi kuyajua hapo hapo au siku hiyo. Kama unataka kununua simu ya zamani ni vyema kununua simu ambayo sio ya zaidi ya miaka mitatu au minne kutoka mwaka uliopo, kwa mfano kwa mwaka huu 2016 unaweza kununua Samsung Galaxy Note 3 au simu nyingine kama hizo.
- Chunguza Vitu ya Ndani Kabla ya Vya Nje
Hakikisha unachunguza vitu vya ndani vya simu kwanza kabla ya kuchunguza vya nje, kwani watu wengi hupenda kutengeneza muonekano wa nje ili simu iweze kuuzika haraka, ukianza kuangalia muonekano wa nje kwanza utajikuta umependa simu hiyo kabla huajajua mambo mengine ya ndani ambayo ni muhimu. Hivyo ni muhimu kuanza kuangalia vitu vya ndani vya simu kama speaker, mic, camera zote ya mbele na nyuma, headphone kama inafanya kazi, Loudspeaker, Network, chaji kama inapokea na pia hakikisha unapiga simu kwa mtu ili kujua kama mnasikilizana vizuri.
- Chunguza Vitu vya Nje kwa Umakini
Hapa ni lazima uwe makini na usiishie kwenye kava tu, hakikisha unaagalia kama sehemu zilizofungwa zinaonekana kufungwa vizuri. Kama simu inaonekana kufunguliwa usikubali kabisa kununua simu hiyo haijalishi muuzaji atakwambia nini, kwani simu nyingi zilizofunguliwa huishia kuwa na matatizo baadae na hii itakusababishia gharama zaidi. Pia ni vizuri kuangalia kioo cha simu hiyo kwa makini ikiwa pamoja na vibonyezo vyote, jaribu kuzima na kuwasha simu hiyo pia bonyeza vibonyezo vyote kama vinabonyezeka inavyotakiwa ikiwa na vibonyezo vya kuandika meseji.
- Hakikisha Simu Unayotaka Kununua ni Halisi (Original)
Kuna njia nyingi za kuangalia simu feki, lakini kwa hapa Tanzania kwa mujibu wa TCRA simu feki zimesha fungiwa, lakini ni vyema kuwa makini kwani bado simu feki zipo na zingine zimeboreshwa zaidi na kuwa karibia sawa na original, hivyo usipokuwa makini unaweza kununua simu ambayo ni feki. Njia rahisi ni ku Google namna ya kujua simu feki ya aina unayotaka kununua kwa mfano unaweza ku Google “how to know a fake samsung galaxy s7″ hapo utaweza kuona njia mbalimbali za kugundua simu feki ya aina unayotaka kununua. Pia unaweza kutumia njia nyingine Hapa.
Kwa kufuata hatua zote hizo utakuwa umefanikiwa kupata simu bora iliyotumiaka na ambayo unaweza kuitumia kwa muda mrefu kidogo. Kumbuka ni vyema kununua simu mpya kwani kuna faida nyingi za kununua simu mpya kama vile, kuweza kurudisha simu inapopata matatizo ndani ya muda fulani (warrant) pamoja na kupata vifaa vyote vya simu yako kama vile chaja, headphone na vifaa vingine.
Blog ipo vizur sna na SoMo limelewka