Hivi unajua kuwa pale unapotoa ruhusa kwa apps mbalimbali kutumia kamera au mic ya simu yako, app hizo zinaweza kuendelea kutumia mic au kamera muda wowote bila hata wewe kujua.?
Yap! kama ulikuwa hujui sasa utakuwa umejua. Ukweli ni kwamba ni ngumu sana kuweza kuthibiti usalama wa simu zetu kwa asilimia 100, kwani inawezekana muda wowote unapokuwa unatumia simu yako kuna mtu ana kusikiliza au anakuangalia kupitia kamera ya simu yako.
Kuliona hilo leo nimekuandalia makala fupi ambayo inaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kutambua kama kuna app ambayo inatumia Mic na Kamera kwenye simu yako bila wewe kujua.. Njia hii ni maalum kwa watumiaji wa Android lakini pia kwa watumiaji wa iOS njia kama hii inakuja siku za karibuni.
Basi kwa kusema hayo moja kwa moja twende kwenye njia hii. Kwa kuanza unatakiwa kuingia kwenye soko la Play Store kisha pakua app inaitwa Access Dots, unaweza kupata app hii hapa au unaweza kudownload kupitia hapo chini.
Baada ya download app hii sasa unaweza kuwasha app hii kwa kubofya kitufe cha Switch kinacho onekana pale unapowasha app hii kwa mara ya kwanza.
Baada ya kubofya utaplekwa kwenye ukurasa wa accessibility ili kuweza kuwasha app hii kupitia sehemu hiyo. Tafuta jina la app hiyo (huwa mwisho kabisa) kisha bofya na washa app hiyo kupitia sehemu hiyo.
Baada ya hapo sasa utaweza kuona kuna kidoti kidogo cha kijani ambacho kitakuwa kinatokea upande wa kulia juu pale app yoyote inakuwa inatumia Mic au Kamera ya simu yako bila wewe kutoa ruhusa. Unaweza kuongeza ukubwa wa kidoti hicho kupitia kwenye sehemu ya settings ndani ya app hiyo.
Mpaka hapo natumaini utakuwa umeweza kuweka ulinzi angalau kidogo wa kutambua kama kuna app ambayo inawasha kamera au mic ya simu yako bila wewe kujua. Kama unataka kuendelea kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua, kama kuna mtu anasoma meseji zako bila wewe kujua. Kwa Maujanja zaidi hakikisha unaiunga na channel yetu kupitia mtandao wa YouTube kwani kuna kitu kipya na kizuri kunakuja siku za karibuni.