Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi ni lazima unajua kuwa, kuna wakati apps ambazo ume install kwenye simu yako zinaji update zenyewe bila hata wewe kuruhusu.
Mara nyingi hii ni tatizo hasa kwa watu ambao unakuta wana MB chache kwenye simu na wanataka kufanya vitu mbalimbali tofauti na ku-update apps hizo.
Sasa kuliona hili leo tumekuletea njia usahihi ya kuweza kuzima (Auto Update) kupitia simu yako ya mkononi ya Android, njia ambayo haifanani na ile njia ya kuzima update za apps zote kupitia sehemu ya settings kupitia soko la Play Store.
Kama kwa namna yoyote unataka kutumia njia ya settings unaweza kuipata kupitia settings kwenye soko la Play Store.
TABLE OF CONTENTS
Jinsi ya Kuzuia Auto-update
Kwa kuanza bofya sehemu ya Profile ndani ya app ya Play Store, kisha baada ya hapo moja moja utaona Menu mpya ikifunguka.
Baada ya Menu hiyo kufunguka, moja kwa moja endelea kwa kuchagua sehemu ya Settings iliyopo mwisho kabisa kwenye Menu hiyo.
Baada ya hapo moja kwa moja fungua menu hiyo ya Settings kisha tafuta sehemu iliyo andikwa Network preference.
Baada ya kubofya sehemu hii moja kwa moja utaweza kupata Menu nyingine zaidi ambazo zitafunguka kwa chini. Tafuta Menu iliyoandikwa Auto-update apps.
Baada ya kubofya sehemu hiyo sasa chagua sehemu ya Don’t auto-update apps, sehemu hii ni ya mwisho kabisa kwenye menu hii.
Baada ya kuchagua sehemu hiyo malizia kwa kubofya sehemu ya Done inayopatikana kwenye kuona ya kulia chini.
Kwa kufanya hatua hizo zote utakuwa umezuia apps kuweza kuji update zenyewe na kumaliza data yako hata kama ume unganisha simu yako kwenye Wi-Fi.
Jinsi ya Kuzuia Auto-update kwenye App Moja
Mbali na njia hiyo kama hutaki kuzuia app zote kuweza kuji update na unataka kuzuia app moja maalum ku-update unaweza kufuata njia zifuatazo.
Ingia kwenye soko la Play Store kisha nenda kwenye app ambayo unataka kuzuia updates, kisha bofya vimishale vitatu vilivyoko juu upande wa kulia kisha
Baada ya hapo utaona sehemu imeandikwa “Enable auto update”, ondoa tiki kwenye sehemu hiyo na utakuwa umemaliza. Rudia hatua hii kwenye kila app ambayo unataka kuzima Auto update.
Jinsi ya Ku-update Apps Zote Baada ya Kuzima Auto-update
Kama unataka ku-update apps zote kwa pamoja unaweza kutembelea Menu kwenye profile yako ya Play Store kisha chagua sehemu ya Manage apps and device.
Baada ya hapo chagua sehemu ya Update all ambayo inapatikana chini ya Menu ambayo imeandikwa Updates available.
Uzuri wa njia hizo ni kuwa utaendelea kupokea meseji za kukujulisha kuwa unatakiwa ku-update apps lakini apps hizo hazitoweza kuji-update zenyewe hadi hapo wewe utakapo ruhusu.
Natumaini makala hii fupi itakusaidia kuweza kuzima Auto Updates kwenye apps mbalimbali kupitia soko la Play Store. Kumbuka unaweza kutumia njia zote mbili ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi na kuhakikisha update zimezima kikamilifu.
Kwa maujanja zaidi hakikisha una Subscribe kwenye channel yetu ili kuweza kifunza maujanja kama haya kwa vitendo. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.
Napenda elimu ya tech
Karibu sana