Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Wezesha (PIP) Picture in Picture Kwenye Video Yoyote (Chrome)

Angalia video bila kufungua kupitia ukurasa mwingine wa tofauti
Wezesha (PIP) Picture in Picture Kwenye Video Yoyote (Chrome) Wezesha (PIP) Picture in Picture Kwenye Video Yoyote (Chrome)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kufanya kazi kwenye kompyuta yako huku unaangalia video basi makala hii ni kwaajili yako. Kupitia njia hii nitakuonyesha jinsi ya kuwezesha PIP au Picture in Picture Mode kwenye video yoyote kupitia Chrome.

Kitu cha muhimu ni kuhakikisha kuwa unatumia browser kwenye kifaa chako hapa na maana computer (desktop au laptop) yenye kutumia mfumo wa Windows.

Advertisement

Kama tayari unayo yote hayo basi moja kwa moja utaweza kuendelea kwenye hatua inayofuata. Kwa kuanza unatakiwa kuona jinsi PIP au picture in picture inavyofanya kazi. Kwa mfano mimi wakati naandaa makala hii nimekuwa nikiangalia series kupitia Netflix huku nikiandika makala hii.

Wezesha (PIP) Picture in Picture Kwenye Video Yoyote (Chrome)

Kama unavyoweza kuona hapo juu unaweza kuangalia video bila kuwa umehama kwenye kazi au kitu unachofanya. Unaweza kuweka video juu ya kitu chochote iwe ni app kwenye kompyuta yako au sehemu yoyote ile ndani ya PC yako.

Basi baada ya kujua jinsi PIP inavyo onekana kwenye kompyuta yako basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwenye hatua jinsi ya kuwezesha sehemu hii kwenye kompyuta yako.

Hatua ya kwanza, bofya hapo chini na utapelekwa kwenye extension store ambao unatakiwa kupakua na kuinstall extension. Bofya hapo chini kupakua moja kwa moja.

Baada ya hapo moja kwa moja unaweza kuendelea kwa kufuata hatua hapo chini na utaweza kuwezesha picture in piture kwenye browser yako ya chrome kupitia kompyuta. Sehemu hii inafanya kazi kwenye video yoyote iwe Netflix, Youtube au mtandao mwingine wowote.

Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu browser ya Chrome unaweza kusoma hapa kujua njia mpya mbalimbali za kutumia Chrome kwenye simu yako ya Android. Kwa maujanja zaidi hakikisha una tembelea Tanzania tech kila siku, pia pakua app yetu kupitia hapa. Usisahau kubadili lugha kwende kiswahili ili kupata makala zetu za kiswahili.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use