Ni wazi kuwa hapa Tanzania watu wengi sana wanamiliki channel za YouTube, kadri watu wanavyozidi kuwa na channel ni wazi kuwa ni watu wengi sana wana hitaji msaada wa YouTube.
Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuchat na YouTube moja kwa moja bila kupitia njia ndefu au kuandika email.
Kupitia njia hii utaweza kuchat na mfanyakazi wa YouTube, na utaweza kusaidiwa tatizo lolote ambalo utakuwa nalo kwenye channel yako. Kitu cha muhimu ni kujua kuwa unahitaji kuwa na link ya channel yako kabla ya kuanza kuwasiliana na YouTube moja kwa moja.
Unaweza ku-copy link ya channel yako kwa kutembelea channel yako, na pia hakikisha link yako inakuwa kwenye mfumo kama unaofanana na mfano hapo chini.
https://www.youtube.com/channel/UCkRfArvrzheW2E7b6SVT7vQ
Baada ya kupata link ya channel yako, sasa moja kwa moja endelea kwa kutembelea link hapo chini kisha fuata hatua zifuatazo. Hakikisha unafuata hatua hizi kwani bila kufuata utaweza kujibiwa na roboti na sio mtu binafsi ambaye anaweza kukusaidia kwa haraka zaidi.
Ukifika kwenye fomu hii, kitu cha kwanza utakutana na swali linalo uliza “Tell us what we can help with:” hakikisha chini yake una andika “Support“. Usindike alama za koma, andika kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.
Baada ya hapo bofya Next, na baada ya hapo litatokea swali lingine ambalo limeandikwa “Choose the best description of this issue:” hakikisha una chagua “Other” ambayo ipo mwisho kabisa.
Baada ya hapo bofya Tena Next step, kisha utaletewa mada mbalimbali ambazo zinaweza kuhusiana na tatizo lako. Bofya Next step na usichague mada yoyote. Kumbuka hii ni muhimu sana kama unataka kuchat au kuwasiliana na YouTube moja kwa moja.
Baada ya hapo moja kwa moja kama umefuata hatua zote unaweza kuona sehemu ya kuchat Live na YouTube moja kwa moja na mtoa huduma au mfanyakazi wa YouTube. Hakikisha unabofya sehemu ya Live Support ili kuchat na mtoa huduma.
Baada ya kubofya sehemu ya Chat moja kwa moja subiri baada ya sekunde chache na utaletewa sehemu ya kuweka link ya channel yako ambayo ina tatizo na kisha bofya Start chat.
Baada ya kubofya Start chat, moja kwa moja utaweza kuona sehemu ya kuchat ikifunguka na utaweza kuchat na YouTube moja kwa moja na kueleza tatizo lako na watakusaidia.
Kitu cha muhimu kufahamu ni kuwa, hakikisha unatumia njia hii kama unalo tatizo kwenye kwenye channel yako. Kwa kutumia njia hii vibaya unaweza kufungiwa channel yako kwa muda mfupi.
Pia kuna uwezekano mkubwa usiweze kuona kupata huduma ya kuchat na mtu moja kwa moja hasa kama channel yako ni mpya sana au imekiuka vigezo na masharti ya YouTube. Kumbuka njia hii ni haitumiki kutoa taarifa mbalimbali bali ni kupata msaada kwa channel yako pekee hivyo kuwa makini unapo tumia njia hii.
Kwa kufata maelezo haya na imani utakuwa umeweza kuwasiliana na huduma kwa wateja au kuwasiliana na YouTube moja kwa moja.