Jinsi ya Kutumia Programu ya VLC Ku-Convert Video ya Aina Yoyote

Convert video zako kwa urahisi bila programu ya ziada
VLC-Media-Player VLC-Media-Player

Wote tunaijua programu ya VLC kuwa ni programu ya kuangalia video na kusikiliza audio, lakini ukweli ni kuwa programu hii inauwezo wa kufanya mambo mengi zaidi ya vile tunavyodhani. Kama unatembelea Tanzania Tech mara kwa mara utakua unajua baadhi ya vitu ambavyo programu hii inauwezo wa kufanya. Kwa siku ya leo tunakuletea jinsi ya kutumia programu hii ya VLC ku-convert video ya aina yoyote kwa urahisi na haraka.

Moja kwa moja twende tukajifunze hatua kwa hatua njia hii rahisi, Kwa kuanza kama huna programu ya VLC hakikisha unadownload kupitia tovuti ya videolan.org kisha install programu hiyo kwenye kompyuta yako alfu endelea kwa kufuata hatua hizi.

Advertisement

Bofya sehemu ya Media iliyoko juu upande wa kushoto kisha chagua Convert/Save baada ya hapo utaona kimefunguka chumba kidogo kinachokutaka kuweka video unayotaka ku-convert, bofya Add kisha chagua video yako unayotaka ku-convert alafu bofya Open kisha baada ya hapo bofya Convert Save kisha chagua aina ya video unayotaka iwe kisha andika jina la video yako kwenye Destination file kisha malizia kwa kubofya Start. Baada ya hapo utaona kuna mtari unapita chini kama vile unaagalia video kisha baada ya hapo utakuwa umemaliza.

Kwa kutumia njia hii unaweza ku-convert video kuwa audio yaani MP3 hivyo kama kuna video unaipenda na ungependa kuisikiliza kwenye simu yako sasa unaweza kufanya hivyo kwa urahisi kwa kutumia programu yako ya VLC. Kama unataka kujifunza maujanja mengine kuhusu VLC unaweza kutafuta hapo juu kwa kuandika “VLC” na utapata kujua mengi kuhusu programu hiyo yenye uwezo zaidi ya kazi yake ya kawaida ambayo imezoeleka.

Kwa habari zaidi za teknolojia Download sasa App ya Tanzania Tech ili kupokea habari kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube ili kujifunza maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use