Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tumia Kamera ya Simu Kama WebCam ya Kompyuta

Kompyuta yako haina WebCam..? tumia njia hii rahisi
simu ya android kama webcam simu ya android kama webcam

Ni kweli kwamba kuna wakati unahitaji kamera ya kompyuta hii inaweza ikiwa ni kwa ajili ya kazi au kwa ajili ya mambo mengine ya muhimu.

Kama unayo kompyuta lakini haina sehemu ya webcam makala hii itakusaidia kubadilisha kamera ya simu yako kuwa kamera ya kompyuta maarufu kama WebCam. Basi bila kupoteza muda twende tuka jifunze hatua kwa hatua.

Advertisement

Hatua ya kwanza unahitaji kudownload programu ya DroidCam programu hii inapatikana kwa kulipia na pia inapatikana bure, unaweza kuchagua toleo unalohitaji kulingana na uwezo wako. Unaweza kupakua programu ya bure kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hiyo ya DroidCam kwenye simu yako ya Android sasa endelea kwenye hatua inayofuata.

Kwenye hatua inayofuata pakua programu nyingine kwaajili ya kompyuta yako, unaweza kupata link ya programu hiyo hapo chini.

Download Programu Hapa

Baada ya kupakua programu hiyo na kuinstall kwenye kompyuta yako sasa endelea kwenye hatua inayofuata.

Baada ya kuinstalll programu ya DroidCam kwenye kompyuta yako ifungue na utaletewa sehemu yenye kutaka uweke Device IP.

Ili kupata Device IP fungua App ya DroidCam kwenye simu yako kisha utaona WiFi IP zinazo onekana kwenye app hiyo. Andika namba hizo kwa usahihi pamoja na nukta zake kwenye kompyuta yako kwenye sehemu ya Device IP.

Moja kwa moja weka tiki sehemu ya Audio kama unataka kuweka na sauti kisha bofya Start kwenye programu hiyo kwenye kompyuta yako.

Tumia Kamera ya Simu Kama WebCam ya Kompyuta

Baada ya hapo utaweza kuona picha ya kwenye simu yako kupitia kompyuta yako, unaweza kubadilisha mpangilio kwa kuchangua kuunganisha simu yako kwa waya au kwa kutumia WiFi.

Kwa kutumia waya bofya sehemu ya pili juu kushoto na unatakiwa kutumia waya wa simu yako kuweza kuona picha kwenye kompyuta yako.

Mpaka hapo utakuwa umeweza kuweka webcam kwenye kompyuta yako kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kumbuka programu hii hatumi internet hivyo unaweza kuitumia kwa muda wowote ule.

Kama unataka kujifunza zaidi jinsi ya kutumia simu yako kivingine, unaweza kusoma hapa jinsi ya kuinstall mfumo wa Windows kwa kutumia simu yako ya Android.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use