Hivi karibuni Instagram ilitangaza sehemu mpya ya Insta live, sehemu ambayo kwa sasa imekua maarufu sana kutokana na kutumiwa na watu mbalimbali ikiwemo wasanii wakubwa kutoka ndani na nje ya tanzania. Kutokana na hilo leo Tanzania Tech tunaenda kuangalia jinsi ya kutumia sehemu hiyo ya insta live pamoja na mambo mengine kuhusu sehemu hiyo mpya ya instagram.
Kwa kuanza tuangalie jinsi ya kutumia sehemu hiyo ya Insta Live, ili kutumia sehemu hiyo hakikisha una bando ya kutosha kisha ingia kwenye programu ya instagram kisha bofya kitufe cha kamera kilichopo upande wa juu kushoto, kisha bofya palipo andikwa Live (chini mwisho wa kioo cha simu yako) alafu bofya Start Live Video. Moja kwa moja marafiki zako watapata ujumbe kuwa umeanza kutumia Insta Live.
Baada ya kuanza kutumia sehemu hiyo kwa upande wa juu kulia utaona idadi ya watu wanao angalia video hiyo moja kwa moja kutoka Insta Live, kwa chini yatakua yakipita maoni mbalimbali ya marafiki zako kuhusu video hiyo. Ukisha maliza video yako bofya sehemu iliyo andikwa End iliyopo juu upande wa kulia kisha maliza kwa kukubali, kumbuka baada ya kumaliza video yako video hiyo haitoweza kuonekana tena sehemu nyingine yoyote kwenye programu hiyo ya Instagram.
Kingine kuhusu sehemu hiyo ni kuwa huto weza kutumia sehemu ya Insta Live kama akaunti yako imetengenezwa hivi karibuni yaani kama akaunti yako ni mpya, hivyo ni vyema kungoja kidogo au ingia kwenye tovuti ya Instagram ya msaada ili kupata suluhisho la tatizo lako.
Kwa habari zaidi download App ya Tanzania Tech kupitia play store ili kupata habari kwa haraka na kwa urahisi kila siku, pia unaweza kujiunga na Tanzania tech kupitia mtandao wa Youtube ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.