Jinsi ya Kutuma na Kupokea SMS kwa Kutumia Kompyuta

Jifunze njia ya kukusaidia kutumia kompyuta kutuma SMS
Jinsi ya Kutuma na Kupokea SMS kwa Kutumia Kompyuta Jinsi ya Kutuma na Kupokea SMS kwa Kutumia Kompyuta

Habari na karibu kwenye maujanja, leo tutaenda kuangalia njia mpya ya kukusaidia kutumia na kupokea ujumbe mfupi au SMS kwa kutumia kompyuta yako. Zipo sababu nyingi zinazoweza kukufanya uhitaji kutuma na kupokea ujumbe mfupi kwa kutumia kompyuta, moja ya sababu hizo ni pale unapokuwa unafanya kazi kwenye kompyuta yako.

Ukweli ni kuwa ni ngumu sana kutumia vifaa viwili kwa wakati mmoja tena hasa pale unapokuwa kwenye mazingira ya kazi, vilevile ofisi nyingi hapa Tanzania hazipendi tabia ya kushika simu huku unafanya kazi, sasa kama wewe umekuwa ukipata shida ya namna hii njia hii itakusaidia na utaweza kutumia simu yako kwenye sehemu ya SMS kwa kupitia kompyuta yako.

Advertisement

Njia hii haitaji uwe na ujuzi wowote bali inakuitaji tu uwe unatumia kisakuzi au Browser ya Google Chrome, vilevile unatakiwa kuwa na simu yako Android na bila kusahau kompyuta yako ya mfumo wowote wa Windows PC au hata Mac PC. Kama una mambo yote haya unaweza kuendelea kwa hatua zifuatazo.

Kwanza chukua simu yako ya Android kisha pakua App ya MightyText hapo chini na install vizuri kwenye simu yako. Baada ya kuinstall ingia kwenye kompyuta yako kisha install extensions ya MightyText ambayo nayo pia inaptikana hapo chini, kisha baada ya hapo endelea kwa kufuatilia maelekezo marahisi kwenye video hapo chini.

Download App Hapa

Download Extension Hapa

Baada ya kumaliza njia hizo zote na ukakika utakuwa umeweza kutuma na kupokea meseji kwa kutumia kompyuta yako. Basi kama kuna mahali umekwama au kama una maoni, ushauri au mashwali unaweza kutuandikia hapo chini kwenye sehemu ya maoni, Mpaka siku nyingine endelea kutembelea Tanzania Tech Byee!.

1 comments
  1. njia ipi unaweza kuongeza idadi ya massage kuchart kwenye mighty text kutoka kwenye massage 125 bila kulipiaa kwa mweziiii. nipe maujanjaa hayoooo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use