Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac

Hii hapa njia mpya kutuma na kupokea mafile bila kutumia njia za waya, bluetooth
Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac

Niwazi kuwa kama wewe ni mtumiaji wa simu au kompyuta kwa namna yoyote umekuwa ukitumia njia mbalimbali za kuhamisha au kutuma mafile kwa kutumia njia za Bluetooth, au kwa kutumia waya.

Lakini unajua kuwa kuna njia nyingine ambayo ni bora zaidi na inaweza kusaidia kutuma mafile kutoka kifaa chochote kwa urahisi..? Kupitia makala hii nitakuonyesha njia hii ambayo pengine ndio njia bora kwa sasa ya kutuma mafile kwa haraka zaidi.

Advertisement

Kwa kuanza unatakiwa kupakua app hapo chini, Kwa watumiaji wa Android pakua kutoka kwenye soko la Play Store, App Store kwa watumiaji wa iPhone au Kama unatumia Windows au Mac unaweza kupata app hii kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa Kupakua App Hii

Baada ya kupakua app hii hakikisha una install kwenye vifaa vyote viwili, kama unataka kutumia mafile kati ya kompyuta na simu basi hakikisha simu na kompyuta zote zinayo programu hii kisha moja kwa moja endelea kwenye hatua inayofuata.

Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac

Kupitia kifaa kimoja wapo Washa Hotspot na unganisha na simu au kompyuta unayotaka ipokee mafile, Huna haja ya kuwa na Data kwenye simu yako au kompyuta.

Baada ya hapo fungua programu uliyo install kwenye simu zote mbili utaona majina ya simu zote mbili na sasa utaweza kutuma mafile kwa haraka zaidi kati ya simu na kompyuta au simu na simu.

Kupitia app ya simu ambayo unataka kutuma file lolote bofya sehemu ya Send, kisha utaona jina la simu ambayo unatala iweze kupokea file, kwa mfano huu mimi kama unavyoona kwenye picha ni “Fine Blueberry”.

Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac

Chagua aina ya file unalotaka kutuma kwa kubofya aina ya file juu, chagua File kama unataka kutuma mafile ya aina mbalimbali, chagua Media kama ni picha na video na audio, chagua Text kama unataka kutuma maandishi na Folder kama unataka kutuma file.

Chagua simu au kifaa unachotaka kisha malizia kwa kukubali kupitia kwenye simu ya pili au kifaa chochote unachotaka kupokea file.

Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kutuma mafile kupitia vifaa mbalimbali bila kutumia waya au Internet. Uzuri wa njia hii inafanya kazi kwenye simu zote yaani Android na iOS pia Windows OS na hata Mac OS.

Kama kwa namna yoyote utakuwa umekwama unaweza kuuliza kupitia maoni hapo chini au kupita WhatsApp moja kwa moja tutakusaidia. Kwa maujanja zaidi hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech kupitia soko la Play Store ili kujifunza zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use