Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii basi ni lazima unafahamu kuhusu sehemu ya Stories. Kama hujui sehemu hii ni ile ambayo hupitisha picha na video ambazo huwa kwa mtindo wa wima na ufutika baada ya masaa 24.
Kama ulikuwa unajua kuhusu sehemu hiyo labda niku ulize..? Hivi unajua kuwa sehemu ya Stories kupitia mtandao wa Instagram ina watumiaji zaidi ya Milioni 400 kila siku.? Na hivi unajua kuwa sehemu ya Stories inaweza kukusaidia kupata followers kwa haraka zaidi kuliko post za kawaida.
Baada ya kusema hayo basi kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia bora na rahisi ambayo itakusaidia sana kuweza kutengeneza Stories kwa urahisi na haraka bila kuwa na ujuzi wowote. Njia hii ni bora kwa watu wote uwe mfanya biashara au mtu wa kawaida njia hii ni bora sana.
Kwa kuanza moja kwa moja pakua app kupitia link hapo chini, baada ya kupakua app hiyo Install kwenye simu yako ya mkononi ya Android baada ya hapo moja kwa moja fungua app hiyo.
Baada ya kufungua app hiyo chagua template unayo pendelea zaidi, template hizi ni video hivyo unaweza kusubiria dakika chache na utaona zikicheza au kuplay moja kwa moja. Ukiona ambayo ni bora kwa matumizi yako, moja kwa moja bofya na utaona ina download moja kwa moja kwenye simu yako na utaruhusiwa ku-edit video hiyo.
Baada ya sehemu ya ku-edit kufunguka utalewa sehemu ambazo unatakiwa kuweka picha zako, bofya kwenye sehemu hizo ambazo zinakuwa wazi na app hiyo itafungua gallery kwenye simu yako.
Chagua picha moja au kama template hiyo inaruhusu picha zaidi ya moja chagua idadi ya picha unazotaka kisha bofya sehemu ya juu kwenya kona upande wa kulia na picha hizo zitaweka kwenye Stories uliyo chagua moja kwa moja.
Kama unataka kuedit font unaweza kuchagua kitufe cha A+, pia kama unataka kuweka nyimbo kwenye Stories yako unaweza kubofya kitife cha Muziki na kama unataka kuongoeza au kupunguza muda wa Stories yako unaweza kubofya kitufe chenye alama ya saa.
Baada ya kuweka picha moja kwa moja unaweza kubofya kitufe cha jicho kilichoko katikati juu na utaweza kuona video yako ikicheza moja kwa moja pamoja na sauti na unaweza kudownload moja kwa moja kwenye simu yako.
Ili kudownload unaweza kubofya kitufe cha download kilichopo upande wa kuu kulia kisha moja kwa moja utaweza kuona Stories yako ikihifadhiwa kwenye simu yako. Moja kwa moja ingia kwenye Gallery ya simu yako na utaweza kuona video hiyo.
Kwa kufanya hatua hizo utaweza kutengeneza Stories kwa urahisi na haraka, njia hii ni bora na rahisi na utaweza kutengeneza Stories mbalimbali kwa haraka bila kupoteza muda mwingi. Kama unataka kujifunza zaidi, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza post za mitandao mbalimbali ya kijamii kwa haraka.