Katika ulimwengu wa AI ni wazi kuwa kila sehemu inatarajiwa au imeguswa na mabadiliko haya ya teknolojia. Moja kati ya mabadiliko hayo ni pamoja na mabadiliko ya jinsi muziki unavyo andikwa na kutengenezwa.
Kampuni moja ambayo imejikita kwenye utengenezaji wa Muziki kupitia teknolojia ya AI imetengeneza mfumo ambao mtu yoyote anaweza kutumia kutengeneza muziki ambao unaweza kusikilizwa na mtu yoyote.
Udio ni mfumo mpya wa AI ambao unaweza kutengeneza muziki wenye uwezo mkubwa wa kutambuliwa kama umetengenezwa na binadamu japo kuwa ume tengenezwa na AI, Mfumo huu unaweza kutengeneza kuanzia Beat, Mdundo na hata maneno pia. Unaweza kusikiliza mfano wa kionjo hapo chini.
Uzuri wa mfumo huu unaweza kutengeneza muziki hata kwa lugha ya kiswahili na hata lugha nyingine za kigeni kama kiarabu na nyingine.
Jinsi ya Kutengeneza Muziki kwa AI
Kama umependa ulicho sikia na unataka kutengeneza muziki kama huu kwa kutumia AI basi unaeza kufuata hatua hizi rahisi.
Hakikisha unayo internet kwenye simu yako kisha moja kwa moja tembelea tovuti hapo chini na moja kwa moja tengeneza akaunti ya bure.
Chagua Sign Up kisha chagua Google moja kwa moja utaweza kutengeneza akaunti kwa kutumia akaunti yako ya Google.
Baada ya hapo utapelekwa kwenye uwanja ambapo unatakiwa kuandika maelezo ya muziki unaotaka, unaweza kuandika kwa kingereza (English) huku ukitaka mfumo huu utengeneze nyimbo yenye mashairi ya kiswahili.
Kwa mfano mimi ili kupata nyimbo hiyo hapo juu niliandika prompt hii.
Prompt: Create a Bongo Flava song talks about Audio Mpya
Baada ya kuandika prompt yako vizuri subiri baada ya muda na moja kwa moja utaweza kupata mfano wa kwanza wa nyimbo unayotaka. Kama utakuwa umeridhika na sample ya kwanza unaweza kuongeza nyimbo hiyo kwa kubofya sehemu ya Extend.
Pia unaweza ku publish nyimbo yako Kwaajili ya watu wengine kusikiliza au unaweza kufanya remix ya nyimbo yoyote unayo iona kwenye platform ya Udio.
Na hiyo ndio njia rahisi ya kutengeneza muziki kwa maandishi kwa kutumia mfumo wa AI. Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu AI hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku pia kwa maujanja na habari za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech Kiswahili kila siku.
Pia usisahau kupakua app yetu ya Tanzania Tech kupitia soko la Play Store kisha badilisha lugha kwa kubofya Menu alafu chagua Swahili Site.