Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutengeneza Blog kwa Kutumia Mtandao wa Blogger

Kama unataka kutengeneza blog bora kwaajili ya habari na mengine fuata njia hizi
Kutengeneza Blog Kutengeneza Blog

Kuna mitandao mingi maarufu na inayokupa nafasi ya kuweza kutengeneza blog bure kabisa bila kutumia gharama yoyote, baadhi ya mitandao hiyo ni pamoja na Blogger, WordPress, Tumblr, Joomla, Wix, Weebly na mitandao mingine mingi. Kwa siku ya leo tutaenda kuangali jinsi ya kutengeneza blog kwa kutumia mtandao wa Blogger. Kutokana na somo letu kuwa refu kidogo tutaenda kuligawa kwa vipengele maalumu ili kukusaidia kuelewa zaidi.

Jinsi ya Kujiunga na Mtandao wa Blogger

Advertisement

Kipengele hichi cha kwanza tutaenda kuangalia jinsi ya kujiunga na mtandao wa Blogger, Blogger ni mtandao wa bure kabisa na pia ni huduma inayotolewa na mtandao maarufu wa Google hivyo usiwe na wasiwasi kuhusu malipo.

Hatua za Kufuata

  1. Hatua ya kwanza bofya hapa www.blogger.com au andika link hiyo kwenye simu au kwa kutumia kifaa chako chochote chenye internet.
  2. Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa maalum ambapo hapo uta bofya kwenye kitufe kilichoandikwa Create Your Blog.
  3. Kwa kua mtandao wa Blogger ni sehemu ya huduma za Google utatakiwa kufungua blog yako kwa kutumia email ya mtandao huo yaani Gmail, hakikisha unaingia kwenye akaunti yako ya Gmail kwa kutumia email yako (barua pepe) pamoja na password (nywila) yako. Kama huna akaunti ya Gmail unaweza ukajisajili kwa kubofya Hapa.
  4. Baada ya Hapo utaletwa kwenye ukurasa maalumu ambapo utatakiwa kuandika jina la Blog yako pamoja na address au link ambayo ndio itakuwa maalum kwa blog yako.
  5. Kisha baada ya hapo bofya kitufe kilicho andikwa Create Blog.

Baada ya kukamilisha hatua zote hizo utakuwa umemaliza hatua ya kwanza ya kutengeneza na kujiunga na mtandao wa Blogger, endelea na hatua nyingine zinazofuata.

Jinsi ya Kuweka Kiolezo (Template) Kwenye Blogger

Hapa tutaenda kuangalia jinsi ya kuweka kiolezo au template kwenye blog yako uliyotengeneza kwenye hatua zilizopita. Kumbuka unaweza kuweka template mbalimbali kutokana na muonekano unaotaka au kutokana na mada ambayo blog yako inahusu.

Hatua za Kufuata

  1. Tafuta template mbalimbali kwa kutumia Google kutokana na Mada ya Blog yako, unaweza kutafuta kwa kutumia maneno “Free Blogger Template“.
  2. Download Template kupitia tovuti moja wapo kama vile hii colorlib kisha hifadhi file lako mahali ambapo ni rahisi kuliona hapo baadae.
  3. Baada ya hapo hakikisha unayo programu ya kufungua .zip file kama huna programu hiyo unaweza kudownload Hapa kama unatumia Windows na Hapa kama unatumia Mac.
  4. Baada ya kupakua programu ya kufungua file za .zip nenda mahali ulipo hifadhi file ulilo download kwenye hatua ya pili kisha bofya kitufe cha kulia kwenye mouse yako kisha chakua Extract Here.
  5. Baada ya hapo utapata file lenye format ya html, fungua file hilo kisha Copy code zote zilizoko kwenye file hilo kisha endelea kufuata hatua zinazofuata.
  6. Nenda kwenye uwanja wako wa blogger kisha upande wa kushoto chagua mahali palipo andikwa Template.
  7. Baada ya hapo kwenye box la kwanza kutoka kushoto chagua sehemu iliyo andikwa edit html
  8. Bofya katikati ya kibox chenye Code kisha bofya kwa pamoja Ctrl pamoja na A kwenye keybord yako.
  9. Baada ya Hapo hifadhi mabadiliko kwa kubofya Save Template kushoto.
  10. Baada ya hapo bofya View Blog iliyoko upande wa kushoto juu ili uweze kuona mabadiliko ya blog yako.

Kwa kufuata hatua zote hizo utakuwa umefanikisha kuweka template kwenye blog yako uliyoitengeneza kutoka kwenye mtandao wa blogger.

Jinsi ya Kuanza Kupost kwenye Blog Yako

Kama utakua umefuata sehemu zote mbili za mwanzo basi hapa utakua uko tayari kuanza kupost au kuweka habari kwenye blog yako mpya uliyo itengeneza awali, kumbuka kutumia blog yako kusambaza habari za maana kwani usipo fanya hivyo Google wanaweza kukufungia akaunti yako na kukunyima usifungue nyingine chini ya jina hilo.

Hatua za Kufuata 

  1. Bofya sehemu iliyoandikwa post iliyoko upande wa kushoto wa dashboard ya yako.
  2. Kisha chagua sehemu iliyo andikwa New post iliyoko upande wa kushoto juu kwenye dash board yako.
  3. Baada ya hapo andika Kichwa cha habari unayotaka kupost kisha.
  4. Chini yake kwenye box kubwa anza kupost habari unayotaka kuituma kwa wasomaji wako.
  5. Baada ya kubaliza kuandika chagua sehemu ya kuweka picha kisha bofya kutufe chenye alama ya picha kisha weka picha yako sehemu unayotaka itokee.
  6. Baada ya Hapo bofya Publish ili uweze kutuma habari yako kwa wasomaji wako.

Mpaka hapo utakuwa umefanikisha zoezi zima la kufungua blog kupitia blogger, kuweka template pamoja na kuanza kupost habari kwenye blog yako. Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu blogger endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku au unaweza ku-download App yetu ya Tanzania Tech kupitia Play Store na utapata habari mpya na mafunzo ya teknolojia kila siku.

44 comments
  1. Nashukuru kwa Utaalamu wenu juu ya usanidi wa Blogger lakini ningependa kujua zaidi kuhusu kutengeneza Domain ya blog badala ya kutumia example.Blogger.com iwe example.com

    1. Asante Andrew kwa kutembelea Tanzania Tech, Tutaandika makala inayohusu jinsi ya kuunganisha example.com kwenye mtandao wa blogger. Hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech

      1. Nashukuru kwa msaada wenu nimejifunza mengi,vipi kuna ulazima kabla ya kufungua blog ni lazima nisajili tcra au naweza kufungua nikaanza kupost then utaratb wa kusajili page yangu ukafuata? Naomben mnisaidie tafadhali

    1. Bamba zipo programu nyingi zinazo kuwezesha kufungua file la zip, ingia Play Store kama unatumia Android au kama unatumia iOS ingia App store kisha tafuta “zip” alafu pakua programu hiyo kwenye simu yako.

  2. nimefungua blog kupitia blogger lakini nikiitafuta kupitia simu nyingine au pc nyingine haitokei na wakati mwingine naambiwa nijaribu kuspell vizuri,je nn tatizo ?au inakaa mda gan ili ionekane kwenye devices nyingine kwenye gooogle?

  3. Goodluck simwa ahxante kwa elmu yenu m nimefngua blog xawa lakin kuweka picha ya wasif inagoma af inaandka kuwa inaendshwa na blogge picha za michael

  4. Maelekezo yenu nimeyapenda sana kwan nimejifunza kitu kutokana na nyie mko vizuri mnstusaidia kuongeza maarifa Kila siku

  5. Sorry mim nimejaza hap kweny addrees mwanz kabsa inagoma kila ninavyoandika why na unaweza nisaidia mfano hiyo adress

  6. Asante Sana price kwa kunisaidia kutengeneza blog japokua sijasoma it lakini nimeweza kwa kufata mashart

  7. elimu bora lakini kunafumbo moja namna ya kutengeza pato la kifedha tafadhali eleza kinagaubaga.

  8. Nashukuru kwa msaada wenu nimejifunza mengi,vipi kuna ulazima kabla ya kufungua blog ni lazima nisajili tcra au naweza kufungua nikaanza kupost then utaratb wa kusajili page yangu ukafuata? Naomben mnisaidie tafadhali

  9. Maoni*mimi nina shida kidogo blogu yangu aionekan google nimejitaidi kutumia google search console ila naona kama nashindwa msaada naomba

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use