Ulimwengu kwa sasa umekua sana kiasi kwamba karibia huduma zote unazipata kupitia simu yako ya mkononi, hii imesababisha watoa huduma wote ambao hutoa huduma mtandaoni kulazimika kutengeneza programu (App) kwaajili ya huduma zao, lakini katika kufanya hivyo bado unakutana na changamoto kwani ni lazima kuajiri watu kwaajili ya kufanya hivyo ndio mana leo Tanzania Tech tunakuletea njia hii ya kutengeneza app za android bila kuwa na ujuzi wowote maalum.
Kumbuka hauitaji ujuzi mkubwa kufanya hivi bali unaitajika kuwa na kompyuta yenye uwezo wa kuunganisha internet pamoja na logo na picha mbalimbali za kuweka kwenye programu yako. Ni vyema kuangalia kwanza matumizi kisha ndipo ujue jinsi ya kutengeneza picha na logo za kuweka kwenye App au programu yako, pia ni vizuri kuwa na simu ya android kwaajili ya kutest programu yako kabla ujaamua kuipost kwenye masoko ya Android kama Play Store au Amazoni Store.
Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa ili kutengeneza programu hii ni vyema ukajua unataka kutengeneza programu ya aina gani zifuatazo ni tovuti 10 zitakazo kuwezesha kutengeneza programu mbalimbali kutokana na maitaji yako, lakini sisi tutatumia tovuti ya Adromo kama mfano wetu wa leo.
- Mobile Roadie
- TheAppBuilder
- Appy Pie
- AppMachine
- BiznessApps
- BuzzTouch
- Good Barber
- Kinetise
- Andromo
- Como DIY
Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya Andromo kisha tengeneza akaunti kwenye tovuti hiyo, hakikisha unatumia email au barua pepe ambayo utaweza kuingia kwa muda wowote hii ni muhimu sana kwani programu yako itatumwa kwenye barua pepe hiyo baada ya kumaliza kutengeneza programu hiyo, hivyo hakikisha unatumia email sahihi.
Baada ya kujisajili na kuhakiki akaunti yako ingia kwenye akaunti yako kisha utaona mahali palipo andikwa Create New App bofya hapo kisha utaletewa sehemu ya kujaza jina la project hapo hakikisha una andika jina la programu yako kisha bofya Create, baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ulio andikwa Your App Activities hapo utatakiwa kuweka aina ya vitu ambavyo unataka programu yako ifanye, vitu vyote vinapatikana kwa kubofya sehemu iliyoandikwa Add an Activities ifuatayo ni list ya vitu ambayo utatumia na kazi zake.
- About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
- Audio Player – Hapa utaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
- Contact – Hapa utaweza kuweka anwani yako
- Custom Page – Hapa utaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
- Email – Hapa utaweza kuweka barua pepe
- Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
- Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
- Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
- HTML Archive – Hapa utaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
- Map – Hapa utaweza kuweka ramani
- PDF – Hapa utaweza kuweka file la PDF
- Phone – Hapa utaweza kuweka namba ya simu
- Photo Gallery – Hapa utaweza kuweka picha mbalimbali
- Podcast – Hapa utaweza kuweka mfumo wa Podcast
- RSS Feed – Hapa utaweza kuweka RSS fee ya blog yako
- SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
- Twitter – Hapa utaweka ukurasa wao wa Twitter
- Website – Hapa utaweka tovuti yako
- YouTube – Hapa utaweka ukurasa wako wa Youtube
Chagua aina ya kitu ambacho unataka programu yako ifanye kisha jaza vitu utakavyo ulizwa kisha endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya Style hapo utaweza kuchagua rangi pamoja na aina ya style ambayo unataka programu yako iwe, baada ya hapo endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya dashboard hapo utaweza kuchagua aina ya dashbord unayotaka kutumia kwenye app yako kisha save alafu endelea mbele kwa kuchagua Service tumeruka Monetize kwa sababu kwa hii ni app ya bure hivyo hutoweza kuweka matangazao mpaka hapo utakapo lipia kwenye tovuti hiyo kwa maelezo zaidi bofya hapa.
Tukirudi kwenye sehemu ya Service weka namba yako ya Google Analytics ili kujua watu wangapi wanaangalia vitu kwenye programu yako, kisha nenda hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza app yako, sehemu hii inapatikana kwenye Build chagua sehemu hiyo kisha chagua sehemu ya Build My App Hapo subiri kidogo baada ya muda kidogo utapokea barua pepe yenye link ya kudownload App au programu yako.
Ukimaliza hatua zote hizo utakuwa umamaliza kutengeneza programu yako ya kwanza ya Android bila hata kuwa na ujuzi wowote maalum, kama utakuwa unataka kufanya mabadiliko yoyote unaweza kuingia kwenye akaunti yako kisha fuata hatua hizo hapo juu kisha tengeneza tena app yako, kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini kwenye maoni na tutakuelekeza.
Soma Hapa – Jifunze jinsi ya kutengeneza App ya Android kwa kutumia Simu yako ya Mkononi.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
Hapa kwenye I’m not a robot unafanyaje
Maoni*kutengeneza app mpaka uwe na computer tu au hata smartphone pekee unaweza au ? muongozo wakuu.
Sasa kwa kutumia simu iliyo be Rooted waweza kutengeneza app
Je, kwa kutumia simu iliyo be rooted waweza kutengeneza app au mpaka PC tu
Bola PC waweza kutengeneza app
Naomba kujua,ukitaka kutengeneza App inayo support kwenye kila device ni hatua gan unatakiwa upitie au nivigezo gan unatakiwa uwe navyo ili kuikamilisha iyo App
Asante kwa masomo yenu ila nilihitaji zaidi kujifunza mambo ya graphics hasa adobe photoshop.
Bado hatuja anza kudeal na graphics
Naomba ikiwezekana hata kwa phone no…
Contacts zangu :;
0684507710
0765755357
Naamini huenda ndoto yangu kumbe yaweza timia japo sina ujuzi au elimu juu ya haya mambo,….!
Lakini kwa masomo yenu yana encourage sana… Natumaini mwitikio wenu plz
Nawezaje kuingiza Hela kupitia app niliyoitengeneza ?
Malipo ya ku-host mobileApp kwa mwaka ni kiasi gani Ndugu?…
Naomba kujua app hii nawez kufungulia kwenye sm au mpka compyuta tu na unaingilia wapi
Maoni*mimi naitaji kutuma app kweny play store ila nimeshindwa no.0745248291
ata kulipia nalipia
Maoni*nielekezeni jinsi ya kutuma application play store vzur
0745248291
NIMETENGEBEZA ADROMO APP LAKINI NIKI SEARCH PLAYSTORE SIIONI LAKINI KWENYE SIMU YANGU NINAYO NA NIKISHEA LINK KWA WENGINE HAIFUNGUKI NINI TATIZO
Maoni* nataka niwe app yangu nifanyeje Mimi naomba maelezo
Maoni* maoni naombeni na app yangu kazi zenu nimezielewa ndo ivo
Jinsi ya kutengeneza apps kwa kutumia simu mbona hamuelezei?
Jinsi yakuweka audio kwenye blog nakuweka link ya kudownload msaada wenu plz?
swali*ili kutengeneza app ni lazima uwe na pc!!?
Hapana unaweza kusoma makala yetu nyingine jinsi ya kutengeneza app kwa kutumia smatphone.
Maoni* Ashukuru Kwakazi Yenu Nzur
jinsi ya kuopload vitu msaada
Maoni*je Nawezaje Kutengeneza App
mbona nikisign in inalud kwenye email adress
Maoni* Ataka Kutengeneza App Yangu Kupitia Simu Inayohusu Ufugaji Je Mashaliti Lazima Uwena Email Tu? Nakama Natumia Gmail
Maoni* lazma uwe na email kiongoz
Ndio ni lazima uwe na barua pepe.
Maoni* Wakuu msaada wenu jinsi yaku unlock network ya simu imejifunga nikiweka line inanandikia UNLOCK SIM BLOCK Natamia H uawei Ascend y 300 Tafandar msaada wenu natanguliza shukran!
Ok
Najaribu kufungua account kwenye andromo inaniandikia not verified sjui shida nn
Angalia kwenye barua pepe yako utakuta kuna email umetumiwa, ndani ya hiyo email utakuta kuna link maalum bofya hapo kuhakiki barua pepe yako.
Simu yangu ni blackberry z3 na nyingine Blackberry 10 passport hila whatsApp inagoma yan situmi picha wala video wala muziki kwa nini na nifanyeje
WhatsApp ilitangaza kuacha kufanya kazi kwenye simu hizo
Simu zangu ni blackberry z3 na BlackBerry 10 passport whatsApp azitumi picha wala video pia hata music kwanini na nifanyeje
Nifanyeje sasa hili niendelee kutumia
Bado kwa sasa hatuja jua njia ya kufanya ila tutalifanyia kazi na kuliweka hapa hapa kwenye tovuti yetu. Asante
Afu app yenu inapayikana kwa jina gan nataka niipakue
Tanzania Tech
kiufupi hakuna chamaana kwa sababu hii tovuti ni ya ajabu haina ktu cha maana sana
asante
ahsante mr nimeelewa
Nataka kuja kwenye ofisi zenu kwa msada zaidi VP zina patikana wapi npo dar es alamu
Jina langu ni Saidi mmbaga kwa mawasiliano zaidi namba 0655380417
Da Kiukweli Nimefurah Sana Kupokea Maujuzi
mbona nimejalib kufungua app himeshindikan shida nn
Mbona App inafanya kazi kama kawaida, Tafadhali wasilina nasi kwa msaada zaidi. Unaweza kutumia fomu hapo chini.
mmmmh jmn mbon nimeshindwa
Umekwama wapi Faustine
nimejalibu kutengeza app lakin imegoma kabsa tena mwanzo kwenye sehemu ya kujaza address na passwed naombeni munisaidie jamaa
Mimi naitwa juma je nitawapataje ili mnielekeze face to face na Ada sh. Ngapi?
Nimetengeneza app ila nashindwa kupost chochote nifanyaje
Kivipi..?
User name inanichanganya Mara namba Mara herufi ndogo naombeni mnielekeze
naomba kufaham app ya android ili kupata beat za music
ku create application kwenye simu aiwezekan?
Inawezekana
thank you
Mimi ni daktari wa saratani nataka kutengeneza app ambayo itanisaidia kuelimisha jamii kuhusu saratani
Habari, inawezekana kabisa pia tunaweza kukusaidia kwenye hilo.
Mm natKa kutengeza bllg
Namba zangu ni 0743643847 na 0745115457 nikifika kwenye username inaleta invalid sory naomba mfano wa username na password hili nifungue app kupitia andromo
Maoni*Je ukiwa na app inakupa faida gani?
Anzisheni hata corse za muda mfupi za kutengeneza programu kama animation cartoon app video marker
Habari,
Mnapatikana ofisi zipi na wapi?
Nahitaji maelekezo zaidi
Habari nmeshatengeneza apo tayari ila nakwama jinsi ya kuiapload playstore na kulipia hizo gharama na ngependa kujua ni shilingi ngapi jumla kukamilisha asanteni
Habari samahan me nilikuw nahitaj jinsi ya kuweka/kuyengeneza RS#
Ni rikuwa nauriza kuna app ambayo inaweza futa wino ambao umefunika neno unataka kujua ni neno gani rimeandikwa