Ulimwengu kwa sasa umekua sana kiasi kwamba karibia huduma zote unazipata kupitia simu yako ya mkononi, hii imesababisha watoa huduma wote ambao hutoa huduma mtandaoni kulazimika kutengeneza programu (App) kwaajili ya huduma zao, lakini katika kufanya hivyo bado unakutana na changamoto kwani ni lazima kuajiri watu kwaajili ya kufanya hivyo ndio mana leo Tanzania Tech tunakuletea njia hii ya kutengeneza app za android bila kuwa na ujuzi wowote maalum.
Kumbuka hauitaji ujuzi mkubwa kufanya hivi bali unaitajika kuwa na kompyuta yenye uwezo wa kuunganisha internet pamoja na logo na picha mbalimbali za kuweka kwenye programu yako. Ni vyema kuangalia kwanza matumizi kisha ndipo ujue jinsi ya kutengeneza picha na logo za kuweka kwenye App au programu yako, pia ni vizuri kuwa na simu ya android kwaajili ya kutest programu yako kabla ujaamua kuipost kwenye masoko ya Android kama Play Store au Amazoni Store.
Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa ili kutengeneza programu hii ni vyema ukajua unataka kutengeneza programu ya aina gani zifuatazo ni tovuti 10 zitakazo kuwezesha kutengeneza programu mbalimbali kutokana na maitaji yako, lakini sisi tutatumia tovuti ya Adromo kama mfano wetu wa leo.
- Mobile Roadie
- TheAppBuilder
- Appy Pie
- AppMachine
- BiznessApps
- BuzzTouch
- Good Barber
- Kinetise
- Andromo
- Como DIY
Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya Andromo kisha tengeneza akaunti kwenye tovuti hiyo, hakikisha unatumia email au barua pepe ambayo utaweza kuingia kwa muda wowote hii ni muhimu sana kwani programu yako itatumwa kwenye barua pepe hiyo baada ya kumaliza kutengeneza programu hiyo, hivyo hakikisha unatumia email sahihi.
Baada ya kujisajili na kuhakiki akaunti yako ingia kwenye akaunti yako kisha utaona mahali palipo andikwa Create New App bofya hapo kisha utaletewa sehemu ya kujaza jina la project hapo hakikisha una andika jina la programu yako kisha bofya Create, baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ulio andikwa Your App Activities hapo utatakiwa kuweka aina ya vitu ambavyo unataka programu yako ifanye, vitu vyote vinapatikana kwa kubofya sehemu iliyoandikwa Add an Activities ifuatayo ni list ya vitu ambayo utatumia na kazi zake.
- About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
- Audio Player – Hapa utaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
- Contact – Hapa utaweza kuweka anwani yako
- Custom Page – Hapa utaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
- Email – Hapa utaweza kuweka barua pepe
- Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
- Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
- Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
- HTML Archive – Hapa utaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
- Map – Hapa utaweza kuweka ramani
- PDF – Hapa utaweza kuweka file la PDF
- Phone – Hapa utaweza kuweka namba ya simu
- Photo Gallery – Hapa utaweza kuweka picha mbalimbali
- Podcast – Hapa utaweza kuweka mfumo wa Podcast
- RSS Feed – Hapa utaweza kuweka RSS fee ya blog yako
- SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
- Twitter – Hapa utaweka ukurasa wao wa Twitter
- Website – Hapa utaweka tovuti yako
- YouTube – Hapa utaweka ukurasa wako wa Youtube
Chagua aina ya kitu ambacho unataka programu yako ifanye kisha jaza vitu utakavyo ulizwa kisha endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya Style hapo utaweza kuchagua rangi pamoja na aina ya style ambayo unataka programu yako iwe, baada ya hapo endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya dashboard hapo utaweza kuchagua aina ya dashbord unayotaka kutumia kwenye app yako kisha save alafu endelea mbele kwa kuchagua Service tumeruka Monetize kwa sababu kwa hii ni app ya bure hivyo hutoweza kuweka matangazao mpaka hapo utakapo lipia kwenye tovuti hiyo kwa maelezo zaidi bofya hapa.
Tukirudi kwenye sehemu ya Service weka namba yako ya Google Analytics ili kujua watu wangapi wanaangalia vitu kwenye programu yako, kisha nenda hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza app yako, sehemu hii inapatikana kwenye Build chagua sehemu hiyo kisha chagua sehemu ya Build My App Hapo subiri kidogo baada ya muda kidogo utapokea barua pepe yenye link ya kudownload App au programu yako.
Ukimaliza hatua zote hizo utakuwa umamaliza kutengeneza programu yako ya kwanza ya Android bila hata kuwa na ujuzi wowote maalum, kama utakuwa unataka kufanya mabadiliko yoyote unaweza kuingia kwenye akaunti yako kisha fuata hatua hizo hapo juu kisha tengeneza tena app yako, kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini kwenye maoni na tutakuelekeza.
Soma Hapa – Jifunze jinsi ya kutengeneza App ya Android kwa kutumia Simu yako ya Mkononi.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
vipi kuhusu kutengeneza games za kwenye simu..!?
Inawezekana Tutaweka makala jinsi ya kutengeneza game unaweza kuangalia mfano wa Pic Puzzle Game kwenye Play Store Game hii ni ya kiswahili.
Maoni*NATAKA KUJI FUNZA ZAID KUHUSU UMEME YANI TANESKO
Download app ya Veta Somo
Maoni*Dr mwaky daaa vboko nyie
Karibu Sana
Ongereni sana kwa kutuelimisha mbona hyo app ya kujifunza umeme wa Tanesco haipo kwnye Play store.
Karibu sana, bado inapatika Play Store Tafuta “VSOMO” utaiona.
mock bin
aise nimefuatilia ile ya kuangalia umeme uliwekwa mara ya mwisho mita ya kuchomeka imezima kabisa haiwaki tena.
nimewaelewa kwa somo,, je ni jinsi gani ya kutengeneza application kama Facebook whatsup etc
Elly tunaomba uulize swali lako kupitia forum yetu
Nimejitahidi nimetengeza app kwa kutumia andromo lkn mbona play store haionekani nimekosea wapi.
Na Nikitaka kuanza kupost kwenye hiyo app yangu naanzaje
Mbona kwenye play store haionekani nimekosea wapi
Maoni*inaniambia email yangu imeshachukuliwa sijui kwanin?
Danny pamoja na Symon hii app ni lazima ulipie ili uweze kuitum Play Store vilevile Hata Play Store ili kuwa na akaunti ya kuweka App zako ni lazima ulipie pia.
Nimecreate blog inayohusu muziki na video sasa naomba maelekezo namna ya kuanza kuweka hizo video na audio kwenye hiyo blog hiyo natanguliza pongez kwa masomo yenu mazur na jins mnavyojibu maswali kwa wakat
Asante Adam je blog yako umeitengeneza kwa kutumia paltform gani… Ni blogger au Wordpress..?
sasa nitawezaje ku uplod ikiwa sina debit au credit card?
nina blog yangu lakini sijui jins gani naweza kuigiza kipato kupitia blog
Asanteni sana maana hiki kitu nlikuwa nahitaji sana kukijua . Ila ngoja nijaribu kama nikikwama ntawataarifu.
Nimeelewa vizuri sana maana ni mda mrefu sasa nlikuwa naitaji kujua iki kitu asanten. Ila nikikwama ntawataarifu.
Karibu sana Ezylon
Maoni Mimi napenda kujua jinsi ya kuweka blog kwenye play store he inawezekana? pia muweke application ya nafasi za Nazi kila zinapo toka
Vicent
asanteni elimu yenu nitaifanyikazi ipasavyo na kupata kipato kupitia technolo
Karibu sana Vicent
Vicent
tafadhali naitaji msahada wenu Nina simu yangu iPhone 4s ukiwasha inandika iTunes imeshindika kuflash kwa mafundi mtanisadiaje
Mim naulizaaa…ukitengeneza app na kuituma playstore utafaidikaje.yan faida au manufaaa utayapataje.pia inaweza kugharimu kama sh ngapi..hadi kuituma playstore.
shukrani saana
Karibu sana endelea kutembelea Tanzania Tech
Nashukuru sana kwa Teaching yenu kwa mwanafunzi wadogo wa IT kam mim tunapata kujua vingi san. So salute… Muhimu muzidi kutupa vingi sana.
Karibu sana Yusuph.. endelea kutembelea Tanzania Tech.
Nimetengeneza app lakin nikishaifungua hakuna kitu kinachokuja zaid ya about hapo nn nifanye ni app ya usimamiz wa biashara ya duka
Kuna mahaliutakuwa umekosea, ili tukusaidie vizuri uliza swali lako kupitia forum yetu ya Tanzania Tech Forums.
Je kumaliza procec zote ni sh ngap?
Asante Inagarimu Tsh, ngapi kulipia play stor app niliotengeneza?
Unatakiwa kuwa na akaunti ambayo itakugarimu tsh 65,000
Maoni*Natal kufundishwa jinsi ya kutengeneza app
Maoni*nitafaidikaje na app?
Abdu asante saana Tanzania tech
Karibu sana
nilazima kuajiri watu wa kufanya kazi kwenye app?
pili. mtu anapataje matangazo na picha na maneno ya kuweka kwenye app
Jaman m nkifungua akaunti andromo pale kwenye user name inagoma
Nimewezaa kutengeneza app yangu ilaa kueka post na kupata link mtu mwingne a download nmeshindwa naomba msaada wenu
Hapo ni vigumu kukuelekeza kupitia hapa tafadhali angalia video hapo juu
me nahitaji kuja sjui uko wapi me nipo dar no.0672813624 whatsapp 0743323254
Levocatus ndubhashe
Shida yangu nataka kujua kuhusu HTML Archive,podcast na RSS feed.kwa sijavielewa.
Tafadhali Kama unataka msaada zaidi uliza swali lako kupitia forum yetu bofya hapo juu palipo andikwa forum au tafuta kwenye google “Tanzania Tech Forum”
Je nikitaka kununua app lazima niwe na nn
Maoni*naweza guingiza pesavkupitia app yangu
Nahitaji kutengeneza app ya kulipia …ninafanyaje???
samahani
naomba kupata nafasi
yakufanya kazi
mm ni mwanafunzi wa kidato cha tatu nasoma PCM
kunauwezekano nikaw napiga kazi na shule kweny kampun yenu
naomba unijb kupitia0626814832
ndoto yang nikuw hacker
jina langu
emmanuely sheck bryson mwakilema
Mimi ninatengeneza animation na katuni lakini sina wa kumuuzia
Maoni* NAOMBA MUNI SA IDIE TATIZO ILOLIISHE
nimejaribu kufungua akaunti ya dromo nimeshindwa nimeishia kwenye paswed naomba mnisaidie
Mimi nahitaji nitengeneze app kama vile ya thl,kwa mana nipate malipo kupitia content nitakazoweka
Ninavyojua Mimi ninaweza kuwa na app ili niweze kuiuza play store ninaweza kuongea na mwenye account ya developer Google Sasa naamini ninaweza tengeneza kupitia andromo kisha nikaja kwenu Tanzania tech mkanisaidia kuipandisha kwasababu naamini nyie MNA account na ukiwa na account kupandisha hakuna limit ya kupandisha application ngapi je mnaweza nisaidie 0745018003 my phone number pls
Bossan usijali tutakusaidia kwenye hilo ila kumbuka unapo tengeneza programu kupitia Andromo ni lazima ulipie ili waweza kukupa nafasi ya kuiweka Play Store.
mbona nikijalibu kutengeza inagoma mwanzoni kabisa nimeinga addres na passwed lkn imegoma et imeferi kunin hapo naomba musada wenu tushiliki wote
Naomba kujua ivi wanaouza app za android faida wanaipataje. Naitaji kutengeneza na mimi
Nnataka kuunganisha sauti kwenye beat nifanyeje
Mimi ni ridhwani,
Nnataka kuunganisha sauti kwenye beat
nataka kujua jinsi ya kutengeneza app
Tanzania tunao wataalamu wa kutosha inabidi selikar iwajali na kuwapa kipaumbele..ahsante sana kwa somo zuri
Asante na karibu sana
Kwaiyo ukiwa na simu tu huwezi tengeneza app
Mimi naitwa Fikiri Rashidi nipo Nyang’hwale mkoani Geita,Binafsi nimependa sana Tanzania Tech ila nina maswala binafsi nitawapata wapi!????
Unaweza kuuliza kupitia hapa au page yetu ya Facebook
Maoni* poa nimewaata
unawezaje kuhuza app kwenye Google play?