Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tafsiri Meseji ya WhatsApp kwa Lugha Yoyote

Tafsiri SMS, meseji za WhatsApp, Instagram, Telegram na meseji nyingine zote
Tafsiri Meseji ya WhatsApp kwa Lugha Yoyote Tafsiri Meseji ya WhatsApp kwa Lugha Yoyote

Ni kweli kwamba hakuna mjuzi wa mambo kwa asilimia 100, kila mtu kwa nafasi yake lazima analo tatizo la kuto kujua jambo fulani, kwa mfano binafsi yangu najua lugha ya kiswahili na kingereza kidogo na kuna wakati ni lazima kutumia programu fulani ili kuelewa neno la kingereza kwa ufasaha.

Hii imepelekea leo nikuletee makala ambayo binafsi imekuwa ikinisaidia sana kutafsiri maneno kwenye jumbe mbalimbali ninazo tumiwa kupitia kwenye application mbalimbali.

Advertisement

Najua njia hii inaweza kukusaidia na wewe kwani njia hii sio ya kawaida au kama ile ambayo tuliongelea kipindi cha nyuma ambayo unaweza kutumia kamera ya simu kutafsiri maneno.

Njia hii ni bora zaidi na inakusaidia zaidi pale unapotaka kutafsiri maneno yaliyopo ndani ya application yoyote ile ikiwa pamoja na application kama SMS, Email na programu nyingine kama WhatsApp, Telegram, Instagram DM, na nyingine zote zilizopo kwenye simu yako.

Pia kizuri ni kwamba unaweza kutafsiri lugha yoyote iwe ni kiingereza kuja kiswahili au kiswahili kwenda kiingereza au hata kiswahili kwenda kwenye lugha yoyote.

Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye makala hii ambayo nimekuwekea hatua zote kupitia kwenye video hapo chini. Na uhakika baada ya kuangalia video hii utaenda kufurahia na kuweza kufasiri maneno kwenye programu zote ndani ya simu yako.

Kama umefanikiwa kuangalia video yote basi unaweza kupakua app iliyotajwa kwenye video kupitia link hapo chini. Kama utashindwa kupakua app hiyo kupitia link hiyo unaweza kudownload kupitia hapo chini.

Download App Hapa

Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha hupitwi na maujanja zaidi kwa ku-subscribe kwenye channel yetu hapa kupitia mtandao wa YouTube.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use