Teknolojia imezidi kuchukua nafasi siku hizi, sasa unaweza kuwa na simu yako tu na kuweza kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na hili la kutafsiri lugha yoyote kwa kutumia kamera ya smartphone yako.
Jumapili ya leo nimekuleta njia mpya ambayo unaweza ukawa ulikuwa huijui, njia ambayo itakusaidia kuweza kutafsiri maneno mbalimbali kwa haraka bila kupoteza muda kwa kutumia kamera ya simu yako. Njia hii ni rahisi sana na kizuri ni kwamba unaweza kuendelea kutumia njia hii hata bila ya kuwa na Internet mara baada ya kufanya hatua za awali. Lakini kwa kuanza ni lazima kuwa na internet angalau MB 200 ili kuweza kufanya hatua hizi za awali.
Kwa kuanza unaweza kufanya njia hizi kwa kutumia app mbalimbali, lakini app ambayo mimi ningependa kukushauri ni app ya Google, App hii inapatikana Play Store lakini pia kuna baadhi ya simu ambazo zinakuja na app hii moja kwa moja ndani ya simu unaweza kuipata kwa kuangalia kwenye Folder la Google. Kama huna app hii basi unaweza kudownload kupitia link hapo chini.
Mfumo wa Android
Mfumo wa iOS
Baada ya kupakua na install app hizi vizuri kwenye simu yako sasa fungua apps hizi kisha fuatisha hatua kwa hatua kama ilivyo. Kama ndio mara yako ya kwanza unafungua app hii utaletewa sehemu yenye kutaka kuchagua ni lugha gani unataka kuwa unatafsiri mara kwa mara.
Kwa mfano unaweza kuletewa Engilish kwenda Spanish, unachotakiwa kufanya kama unataka kuwa unatafsiri maneno ya kingereza kuja kiswahili basi chagua Swahili kwenye sehemu yenye Spanish. Kumbuka usisahau kuweka tiki kwenye sehemu ya Translate offline kwani sehemu hii ndio itakusaidia kutumia app hii kutafsiri bila kutumia Internet. Baada ya hapo bofya Finished.
Baada ya hapo sasa utakuwa uko tayari kuanza kutafsiri maandishi yoyote kwa kautumia kamera ya simu yako, sasa endepo unataka kutafsiri neno kwa kutumia kamera ya simu yako bofya kitufe cha kamera kisha elekezea kamera kwenye maneno unayotaka kutafsri na moja kwa moja utapa tafsiri yake.
Unaweza kuona hapo chini app hiyo ikiwa imefanya tafsiri ya baadhi ya maneno ya kingereza kuja kiswahili kutoka kwenye kioo cha kompyuta yangu.
Kama unavyoweza kuona Guys njia hii inafanya kazi vizuri sana na kama ulichagua ile sehemu ya Translate offline basi app hii itapakua lugha unayotaka kutumia (MB 40 kwa Kiswahili) kisha unaweza kuendelea kutumia app hii kutafsiri bila hata kuwa na Internet kwenye simu yako.
Lakini pia zipo app nyingine ambazo unaweza kuzitumia, app hizo ni pamoja na Microsoft’s Translator, Camera Translator, pamoja na All Translator. Unaweza kuzipata app hizi kupitia link hapo chini ili kusudi uweze kujaribu kutumia na hizo.
Kumbuka app zote hizi ni za mfumo wa Android hivyo kama unatumia mfumo wa iOS ni vyema kupakua app ya Google ambayo inapatikana juu kabisa kwenye ukurasa huu. Basi hayo ndio maujanja niliyo kuandalia kwa siku ya leo, kama unata kujifunza zaidi unaweza kutembelea ukurasa wa maujanja hapa pia kwa maujanja zaidi hakikisha una subscriber kwenye channel yetu ili kujifunza zaidi kwa vitendo.
Maoni*naweza vipi kupata setting za internet katika simu yangu T728
Ni simu ya kampuni gani..?