Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Njia hii itakusaidia kupata mawasiliano ya barua pepe ya mtu yoyote
Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao umewahi kujiusisha na shughuli za kiofisi ni wazi kuwa unajua umuhimu wa barua pepe au email. Lakini kuna wakati inakuwa ni ngumu sana kupata barua pepe za watu maalum ambao pengine ungependa kuwasiliana nao kwa namna moja ama nyingine.

Kuliona hili leo Tanzania Tech nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kupata email au barua pepe ya mtu yoyote kwa haraka na urahisi. Njia hii ni nzuri na rahisi sana na unaweza kutumia ili kupata barua pepe au email ya mtu yoyote ya kiofisi au hata ya binafsi.

Advertisement

Kwa kuanza hakikisha unayo internet kwenye simu yako au kompyuta, pia hakikisha unayo akaunti kupitia mtandao wa linkedin, kama unasoma makala hii basi kuna uwezekano mkubwa unayo akaunti kupitia mtandao huo wa kijamii kwa ajili ya wafanyakazi. Kama huna akaunti unaweza kutengeneza kwani haichukui muda mrefu na hii itakusaidia sana.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Jisajili na Linkedin Hapa

Baada ya kumaliza kujisajili au kama tayari unayo akaunti ya Linkedin basi unaweza kuendelea kwenye hatua inayofuata ambapo unahitaji kutengeneza akaunti kupitia mtandao wa Rocket reach, kusajili akaunti kupitia mtandao huu ni rahisi na haraka.

Unaweza kujisajili kwa kutumia sehemu za kujaza email yako na username, lakini kama unataka kufanikisha kwa haraka unaweza kutumia akaunti yako ya gmail au facebook kukamilisha usajili.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Jisajili na Rocket Reach Hapa

Baada ya kukamilisha usajili sasa unaweza kuendelea na kuanza kutafuta email au barua pepe za watu mbalimbali kwa urahisi na haraka. Kupitia tovuti hii kwenye akaunti yako ya bure utapewa awamu 5 za kutafuta barua pepe za mtu kwa urahisi, unacho takiwa kufanya ni kubofya sehemu ya kutafuta kisha ingia kwenye mtandao wa linkedin tafuta jina la mtu au kampuni.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Kwenye mfano huu nimetafuta jina wasafi tv, na moja kwa moja kama unavyoweza kuona nimepata majina mbalimbali ya wafanyakazi au waajiriwa wa kituo cha Wasafi tv. Hatua inayofuata unatakiwa ku-copy link ya profile ya mtu ambae unataka email yake au barua pepe.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Baada ya hapo sasa ingia kwenye mtandao wa Rocket reach na moja kwa moja paste link uliyo copy kupitia mtandao wa linkedin na kisha bofya search.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Subiri baada ya muda mfupi na moja kwa moja utaweza kuona email au barua pepe za mtu uliyekuwa unamtafuta, baada ya kuona matokeo moja kwa moja bofya Get Contact na moja kwa moja utaweza kuona emal au barua pepe ya mtu unae hitaji.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Njia hii ni rahisi na itakusaidia sana kupata email au barua pepe ya uhakika ambayo unaweza kutumia kuwasiliana na mtu ambae ulikuwa unataka kumtafuta kiofisi au kwa jambo binafsi. Kumbuka njia hii unaweza kuitumia bure kwa kutafuta watu watano tu na unaweza kutengeneza akunti kwa kutumia barua pepe nyingine kama unataka kupata nafasi nyingine.

Pia unaweza kulipia vifurushi kwenye tovuti hiyo ambapo unaweza kupata namba za simu pamoja na akaunti za mitandao ya kijamii kwa urahisi kwa kutumia njia hii.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Muhimu : Njia hii ni kwaajili ya watu wanaotaka kupata mawasiliano ya watu kwaajili ya maendeleo, kumbuka usitumie njia hii vibaya kwa namna yoyote kwani ni kinyume na sheria kutumia vibaya mawasiliano ya mtu yoyote. Hatuta husika kwa namna yoyote kama ukitumia njia hii vibaya, njia hii ina lengo la kufundisha na sio vinginevyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use