Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuondoa Matangazo Kwenye Programu za Android

Jifunze jinsi ya kuondoa matangazo kwenye baadhi ya programu za simu yako
Matangazo Matangazo

Matangazo au (Ads) kwenye programu au application ndio chanzo pekee kinacho msaidia mtu kupata kipato kupitia programu yake tena zaidi ni pale unapokuta programu hiyo ni ya bure au (Free), lakini matangazo hayo yakizidi sana yanapoteza ladha ya kutumia programu hiyo na pengine kukufanya kuamua kuacha kabisa kutumia programu hiyo. Kutokana na hilo leo Tanzania Tech tunakuletetea njia hii ya kupunguza matangazo hayo na pengine kuyatoa kabisa kutoka kwenye programu zako za mfumo wa Android.

Kwa kuanza basi ningependa tu kusema kuwa njia hii inaweza kuondoa kabisa matangazo au kupunguza na kwa namna moja ama nyingine kuna wakati unaweza usione matokeo moja kwa moja lakini na uhakika itakusaidia hata kupunguza matangazo hayo. Kwa kuanza unatakiwa kudownload programu inayoitwa Lucky Patcher unaweza kudownload kupitia hapa baada ya kudownload install progarmu hiyo kama bado hakikisha unaweka tiki kwenye Setting > Security > kisha weka tiki palipo andikwa  “Unknown sources” alafu maliza kwa kubofya OK endelea mbele kwa kufungua programu hiyo.

Advertisement

Baada ya Kufungua programu hiyo hakikisha unaacha kwanza imalize kutafuta programu zote na pia kama kuna update za programu hiyo hakikisha una update kwani kwa kufanya hivyo uwezekano wa programu hiyo kufanya kazi unakuwa mkubwa zaidi. Baada ya kumaliza kutafuta utaona programu zote ambazo ziko kwenye simu yako, tafuta programu unayotaka kuondoa matangazo kisha ichague kwa kuibofya alafu chagua Open Menu Patches kisha bofya tena Create Modified APK File kisha chagua APK without Google Ads kisha chagua Rebulid App iliyoko mwisho kabisa wa programu hiyo

Kumbuka usibadilishe kitu chochote na pia wakati programu hii inafanya kazi usiguse kioo cha simu yako kwani kwa kufanya hivyo programu hiyo ita sitisha kutengeneza file lako, hivyo subiri mpaka programu hiyo imalize kazi kisha bofya Go to file kisha chagua programu yako ambayo utaona jina lake kisha bofya Uninstall / Install kitendo ambacho kitaondoa programu hiyo na kuinstall tena programu hiyo hiyo ambayo tayari imesha ondolewa au kupunguzwa matangazo baada ya hapo jaribu tena programu yako utaona imeonda kabisa au kupunguza matangazo kwenye programu yako.

Angalizo ni kwamba sio kila programu inaweza kuondolewa matangazo na programu hii ya Luck Patcher, kutokana na hilo njia hii inaweza isifanye kazi kwenye simu yako kwa asilimia 100 hivyo basi kama njia hii haitaweza kufanya kazi tuandikie kwenye maoni hapo chini nasi tutakusaidia kutafuta njia ambayo itakufaa na kuondoa matangazo kwenye simu yako.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use