Jinsi ya Kununua Ticket ya Ndege Kwa Kutumia Mtandao

Fuata hatua hizi kama unataka kununua ticketi ya ndege ya Fast Jet
Fast Jet Fast Jet

Kutokana na teknolojia kukua kwa sasa watu wengi hununua tiketi za ndege mtandaoni, hii yote ni ili kuepusha kupoteza muda wa kwenda kwenye ofisi husika na matokeo yake kukosa muda muafaka wa kujiandaa na safari. Ndio maana leo Tanzania tech tunakuletea njia rahisi ya kukata tiketi ya ndege (fast jet) kwa kutumia simu au kompyuta yako.

  • Angalia Uwepo wa Nafasi

Ingiza taarifa kuhusu utokako, uendako, tarehe za kusafiri na idadi ya wasafiri kwenye kisanduku cha ‘nunua tiketi’ kilichopo kwenye upande wa kushoto wa mtandao. Bofya ‘endelea’ kuona uwepo wa nafasi.

Advertisement

  • Chagua Pendekezo Lako la Ndege

Nauli zote zilizopo kwenye tarehe ulizochagua zitaonekana kwenye upande wa kulia wa kioo. Ili kuona ndege kwenye tarehe nyingine tafadhali bofya vitufe vya ‘mapema na baadae’ kwa ajili ya ndege zinazoingia na zinazotoka. Mara upatapo ndege unazozitaka, tafadhali zichague kwenye upande wa kulia wa kioo na ubofye ‘endelea’.

Endapo kwa bahati mbaya umechagua ndege ambazo sizo unaweza kufuta kikapu chako upande wa kushoto kioo unaweza kuboresha utafutaji wako kwa kuchagua upya utokapo, uendako, tarehe za safari na idadi ya wasafiri.

  • Ingiza Taarifa za Msafiri

Kama umeridhika na muda wa safari na nauli ulizochagua, bonyeza ‘endelea’.

  • Thibitisha Safari

Jaza taarifa zote muhimu za wasafiri wanaosafiri kwenye tiketi yako. Majina lazima yafanane sawia na yale yaliyoko kwenye hati au nyaraka za kusafiria za wasafiri. Jaza taarifa zako za mawasiliano na tufahamishe iwapo una mahitaji yoyote maalumu.

Ili kuendelea na hatua inayofuata ya kununua tiketi, thibitisha kama umesoma na unakubaliana na vigezo na mashartiya kampuni kabla ya kubonyeza ‘endelea’.

  • Uthibitisho na Malipo

Ukishathibitisha taarifa za wasafiri wote utatakiwa kuchagua njia ya malipo. Unaweza kulipia safari yako kwa kutumia njia yoyote kati ya hizi zifuatazo:

  1. Credit Card au Debit Card
  2. M-Pesa
  3. Tigo Pesa
  4. Kwa pesa taslimu kaunta au kwa Credit card kwenye ofisi yoyote ya fastjet

Kama unalipia katika ofisi za fastjet au wakala, malipo yanapaswa kufanywa ndani ya muda muafaka, yaani ndani ya

  1. Masaa 48 kama unasafiri ndani ya mwezi
  2. Masaa 24 kama unasafiri ndani ya siku 4
  3. Masaa 6 kama unasafiri chini ya siku 4
  4. Saa 1 kama unasafiri ndani ya masaa 24

Ukiwa unachagua aina ya malipo utapokea namba ya kumbukumbu ya tiketi. Tumia namba hiikufanya malipo kama ni katika ofisi ya fastjet au kwa wakala. Kama malipo hayatapokelewa ndani ya muda muafaka, nafasi ya safari itafutwa na hatutaweza kukuhakikishia tiketi kwa bei ya awali.

Makala hii inapatikana kwenye tovuti ya (Fast Jet) Unaweza kupata maelekezo zaidi kupitia tovuti hiyo au kwa kuwasiliana na kampuni hiyo.

Picture Source: Fastjet

8 comments
  1. Maoni*endapo nikiunganishwa kuwa napta habari kupitia njia ya burua pepe, nitajuaje kama nimesha unganishwa?

  2. Maoni*endapo nikiunganishwa kuwa napta habari kupitia njia ya burua pepe, nitajuaje kama nimesha unganishwa?

  3. Naombeni kufahamishwa jins ya kufanya booking ya kwenda from dar to mwanza kwasababu sijui chochote sijawahi kupanda ndege naomba mnifahamishe plz

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use