Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Hatua kwa hatua jinsi ya kupata Blue Tick Instagram
Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge) Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Instagram Verified au Blue Tick ni moja ya vitu ambavyo ni ndoto kwa watumiaji wengi wa mtandao wa Instagram. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao kwa muda sasa umekuwa unahitaji kupata blue tick au verified Badge basi makala hii ni kwa ajili yako.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha hatua rahisi za jinsi ya kupata Blue Tick au Verified Badge kupitia akaunti yako ya Instagram. Kitu cha muhimu hakikisha akaunti yako imetimiza vigezo na masharti na imekuwa ikitumika kwa muda usiopungua wiki moja.

Advertisement

Mahitaji ya Muhimu Kupata Blue Tick Instagram

Yapo mahitaji ya muhimu ambayo unatakiwa kukidhi ili kupata alama ya blue tick kwa kununua kupitia Instagram, yafuatayo ni mambo hayo machache.

  • Hakikisha akaunti yako inatumia na mtu halisi na sio akaunti ya Kibiashara kiotomatick au inayotumia Facebook API au Instagram Graph API.
  • Akaunti yako inatakiwa kuwa Public na sio Private Account.
  • Akaunti inatakiwa isiwe na promotion nyingi kuliko post nyingine za kawaida.

Hatua za Jinsi ya Kununu Blue Tick Instagram

Hatua ya kwanza ingia kwenye ukurasa wako wa instagram kisha bofya sehemu ya Akaunti iliyopo alama ya mtu upande wa kulia chini. Kisha bofya Menu juu yenye Mistari Mitatu.

Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Baada ya kufungua Menu hiyo moja kwa moja bofya sehemu ya Settings and Privacy. Baada ya hapo Bofya sehemu ya Account Center.

Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Baada ya kufungua Menu hiyo moja kwa moja angali mwisho wa ukurasa huo na utaona sehemu mpya ya Meta Verified.

Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Bofya sehemu ya Meta Verified na Moja wa moja utaletewa ukurasa ambao utakuitaji kuweza kulipia ili kupata Blue Tick. Moja kwa moja bofya Subscribe kama uko tayari kulipia, Unaweza kulipia kwa kutumia Mpesa Visa Card au Tigo Pesa Mastercard au hata Airtel Money Mastercard.

Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Baada ya kubofya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wa Confirm Profile, ukurasa ambao utakupa sehemu ya Sign Up ambapo utabofya hapo ili kufanya malipo. Pia ni vizuri kujua kuwa ukipata Blue Tick kwenye mtandao wa Instagram upata alama hiyo pia kwenye mtandao wa Threads.

Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Gharama za Kupata Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Baada ya kufuata hatua zote hizo hatua ya mwisho ya muhimu ni kujua gharama za kupata verified badge kutoka Instagram.

Kwa sasa kampuni ya Meta inatoa alama ya Blue Tick kwa watu wenye akaunti binafsi na sio za kibiashara kwa gharama ya TZS 34,900 kwa Mwezi ambayo hii itakatwa kila mwezi kwenye akaunti yako hivyo kwa mwaka mzima itakuwa ni TZS 418,800 kwa Mwaka.

Jinsi ya Kununua Instagram Blue Tick (Verified Badge)

Kama uko hapa Tanzania gharama hii huongezeka kidogo kwa kuchaji VAT pamoja na gharama nyingine za kufanya miamala hivyo kama unataka kufanya muamala wa kununua alama ya Blue Tick basi weka hadi TZS 40,000 kwenye akaunti yako ili kufanya muamala kukamilika bila tatizo.

Pia hakikisha unacho kitambulisho binafsi kilichotolewa (Government ID) na serikali pale kitakapo itajika.

Kwa kufuata hatua hizo utaweza kupata alama ya Blue Tick kwenye akaunti yako ya Instagram kwa urahisi sana. Kumbuka unaweza kusubiri hadi siku mbili kuweza kupata alama hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use