Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Sifa Kamili za Simu Yako ya Android (Bila Internet)

Je hivi unajua sifa kamili za simu yako ya Android.? Kama hujui soma hapa
Fahamu Sifa Kamili za Simu Yako ya Android (Bila Internet) Fahamu Sifa Kamili za Simu Yako ya Android (Bila Internet)

Ni wazi kuwa siku hizi katika kundi la watu 10 basi lazima utakuta watu saba wanatumia simu za Android, hii inafanya kuwepo na watumiaji wengi wa simu za Android kuliko hata simu za mifumo mingine kama iOS.

Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa watumiaji wengi wa simu za Android ni wazi kuwa sio watumiaji wote wanaojua mambo yote kuhusu simu hizo. Ndio maana Tanzania tech tumejikita kutoa elimu kuhakikisha watu wote wanajua jinsi ya kutumia simu za Android kwa usahihi pamoja na kujua yote ya muhimu kuhusu simu hizo za Android wanazo miliki.

Advertisement

Lakini nadhani wote tunakubaliana kwamba “kwenye kila elimu kunazo changamoto” na changamoto yetu kubwa ilikuwa, kila mtu ana miliki simu ya tofauti ya Android na kutokana na hilo imekuwa ni ngumu sana kuandika makala kuhusu kila simu ya Android ambayo kila mtu anamiliki, lakini sasa tumepata ufumbuzi wa changamoto hii..

Fahamu Simu Yako

Fahamu Sifa Kamili za Simu Yako ya Android (Bila Internet)

Fahamu Sifa Kamili za Simu Yako ya Android (Bila Internet)

Simu yako ni app mpya ya Android ambayo itakusaidia sana kujua sifa kamili za simu yako ya Android BILA KUTUMIA INTERNET ikiwa pamoja na mambo mengine mengi ambayo ulikuwa ufahamu kuhusu simu yako. App hii ni rahisi kutumia na inakuja na na vipengele vyote vya muhimu ambavyo vitakusaidia kujua kuhusu simu yako na sifa zake.

Ndani ya application hii kuna maelezo ambayo yatakuwa ni maalum kwa kila simu ya Android na maelezo haya yatakuwa ni tofauti kwa kila simu. Iwe unatumia simu ya Samsung, TECNO, Infinix au simu nyingine yoyote inayotumia mfumo wa Android app hii itakusaidia kujua kuhusu simu yako.

Fahamu Sifa Kamili za Simu Yako ya Android (Bila Internet)

Mbali ya yote app hii haina matangazo na ukisha ipakuwa huna haja ya kutumia Internet na itaendelea kuwa bure kabisa kutumia na hutosumbuliwa na kitu chochote. Unacho takiwa kufanya ni kupakua app hii na kusubiri itafute sifa za simu yako na moja kwa moja unaweza kuona sifa zote za simu yako kwa lugha adhimu kabisa ya Kiswahili.

Unaweza kupakua app hiyo kupiria link hapo chini, kama link hiyo hapo chini haifanyi kazi kwenye simu yako, basi unaweza kutumia link hapa kupakua app hii kwenye simu yako ya Android.

Download App Hapa

Kama utakuwa una tatizo au kama app hii haijaweza kufanya kazi kwenye simu yako unaweza kuwasiliana nasi tutakusaidia. Kama unataka kujua zaidi kuhusu simu yako unaweza kusoma hapa kujua sifa na bei ya simu yako, pamoja na simu nyingine mbalimbali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use