Kutokana na kuenea na kusambaa kwa virusi vya corona, leo inabidi tukatisha mada zetu za kila siku ili kukuletea wewe mwana teknolojia njia ambazo unaweza kutumia kujilida dhidi ya virusi vya corona. Hadi siku ya leo tarehe 13 mwezi wa tatu mwaka 2020, kwa mujibu wa tovuti ya Aljazeera, na BBC Swahili, virusi vya corona vime gundulika kwa mgonjwa mmoja nchini Kenya.
TABLE OF CONTENTS
Virusi vya Corona ni nini.?
Kwa mujibu wa WHO, Virusi vya corona au Coronaviruses (CoV) ni familia kubwa ya virusi ambayo husababisha magonjwa kuanzia homa ya kawaida kwenda kwa magonjwa mazito kama vile Middle East Respiratory Syndrome (MERS-CoV) na Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS-CoV). Coronavirus (nCoV) ni aina mpya ambayo haijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.
Coronaviruses ni zoonotic, kwa maana zinaambukizwa kati ya wanyama na watu. Uchunguzi wa kina uligundua kuwa SARS-CoV ilipitishwa kutoka kwa paka aina ya civet hadi kwa wanadamu na MERS-CoV kutoka ngamia kupita kwa wanadamu. Bado kuna aina kadhaa za Coronavirus zinazojulikana zinazunguka katika wanyama ambao hawajaambukiza wanadamu.
Dalili za Virusi vya Corona
Kwa mujibu wa WHO, dalili za kawaida za maambukizo ya Coronaviruses (CoV) au (COVID-19) ni pamoja na dalili za matatizo ya kupumua, homa, kikohozi, upungufu wa pumzi na shida ya kupumua. Katika hali kali zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha pneumonia (nimonia), kuishiwa punzi, matatizo ya figo na hata kifo.
Mara chache zaidi, ugonjwa huo unaweza kuwa mbaya kwa watu wazee, na watu walio na hali zingine za matibabu au matatizo ya afya kama vile pumu, ugonjwa wa sukari, au ugonjwa wa moyo, wagonywa hao wanaweza kuwa katika hatari ya kuwa mgonjwa sana pale wanapo pata ugonjwa huu.
Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Corona Virus
Kwa mujibu wa WHO, hadi siku ya leo tarehe 13 mwezi wa tatu mwaka 2020, hakuna chanjo ya kuzuia ugonjwa wa coronavirus (COVID-19). Mapendekezo ya kawaida ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara, kufunika kinywa na pua wakati wa kukohoa na kupiga chafya, kupika vizuri nyama na mayai na pia kuepuka kugusana na kusogeleana na mtu yeyote anayeonyesha dalili za ugonjwa wa kupumua kama kukohoa na kupiga chafya.
Kwa mujibu wa tovuti ya CDC, Ili kuweza kujilinda zaidi na coronavirus (COVID-19), hakikisha na unaosha vizuri mikono yako kwa maji na sababu na pia unaweza kutumia sanitizer inayotokana na alcohol angalau kwa asilimia 60%. Unaweza kujua kama sanitizer inayo angalau alcohol asilimia 60% kwa kuangalia lebo ya bidhaa. Unaweza kujifunza kunawa mikono vizuri kwa maji na sababuni kupitia video hapo chini.
Mengine ya Muhimu
Makala hii inaelezea mambo machache tu, yapo mambo mengi ya muhimu ambayo ni lazima ufahamu, baadhi ya mambo hayo ni pamoja na haya. Mambo haya ni kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Afya Tanzania.
Kama unataka kupata maelezo zaidi jinsi ya kujilinda dhidi ya virusi vya corona, tembelea tovuti ya wizara ya Afya, au unaweza kusoma maelezo zaidi ya kujilinda na ugonjwa huu kupitia tovuti ya WHO hapa. Kama unataka kujua zaidi kuhusu virusi vya corona vilivyo athiri teknolojia unaweza kusoma hapa.
Vyanzo vya Makala Hii
maoni yangu ni hivi kwenye kwenye vituo