Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuinstall Mfumo wa iOS 12 Kabla Haujatoka Rasmi

Mfumo huu utakao install hapa ni mfumo wa iOS 12 Beta kwaajili ya majaribio
Kuinstall iOS 12 Kuinstall iOS 12

Hivi karibuni kupitia mkutano wa WWDC 2018, Apple ilizindua mfumo wake mpya wa iOS 12, mfumo ambao unakuja na maboresho mengi sana pamoja na sehemu mpya mbalimbali ambazo zinafanya simu za iPhone kuwa tofauti kwa mara nyingine tena.

Wakati Apple tayari imesha zindua mfumo huo, lakini bado mfumo huo haujazinduliwa rasmi kwa watumiaji wote wenye simu zenye kuingia toleo hilo jipya la iOS 12. Kama wewe ni mmoja wa watu wenye simu hizo hapo chini na unataka kujaribu mfumo huo sasa hivi kwenye simu yako basi endelea kusoma makala hii.

Advertisement

Njia hii ni rahisi sana na haitaji uwe na kompyuta na pia haitaji wewe kupakua programu nzima na kuinstall baadae. Njia hii ni salama na inafanya kazi kwa asilimia 100 kwa wale wenye simu zenye uwezo wa kuingia mfumo huo wa iOS 12.

Kwa kuanza hakikisha simu yako ya iPhone imechajiwa kwa asilimia angalau 80 au 50 kisha fungua kivinjari cha Safari kwenye simu yako kisha download FILE HILI lina KB 800 tu. Baada ya kupakua file hilo, simu yako itauliza kama unataka kudownload profile bofya Allow kisha bofya Next ingiza password zako alafu bofya Install. Baada ya hapo simu yako ita restart na baada ya hapo nenda kwenye Settings > General > Software Update, subiri simu yako itafute update kisha utaona imepata update hizo, kama umejiunga kwenye WiFi basi unaweza kubofya Download and Install.

Kumbuka toleo hili la iOS 12 ni toleo la majaribio, hivyo utaweza kuona vitu vidogo vidogo ambavyo vitakuwa vinasumbua kwa namna moja ama nyingine. Toleo imara la mfumo huu wa iOS 12 linatoka baadae mwaka huu na pia utaweza kupakua toleo hilo kama kawaida hata kama tayari ulisha install toleo hili la majaribio.

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuinstall mfumo wa iOS 12 kwenye simu yako ya iPhone, kumbuka ni muhimu kufuata hatua zote na ni muhimu kuhakikisha simu yako ina chaji kwa kiwango fulani kabla ya kufanya hatua hizi. Kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini nasi tutakuelekeza moja kwa moja. Pia unaweza kuuliza swali lako kupitia akaunti yetu ya Telegram kupitia hapa t.me/tanzaniatech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use