Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuficha SMS na Call Logs za Mtu Kwenye Simu ya Android

Kama unataka kuficha meseji au call log za mtu maalum fanya hivi..
SMS na Call Logs SMS na Call Logs

Faragha au usiri ni kitu cha msingi sana iwe wewe ni mfanyabiashara au mtu yoyote yule mwenye nyadhifa yoyote kuwa na faragha ni moja kati ya vitu ambavyo ni muhimu sana. Katika ulimwengu wa sasa wa smartphone au simu janja, kuna wakati unakuta ni ngumu sana kuwa na faragha kwenye simu yako ndio maana leo Tanzania tech tunakuletea jinsi ya kuficha sms na call logs za mtu maalum kwenye simu yako ya Android.

Bila kupoteza muda twende tukaangalie njia za kufanya ili uweze kuficha namba ya mtu maalum kwenye simu yako hiyo ya Android. Kwa kuanza hakikisha unatumia simu yenye mfumo wa android ya toleo la 4.0 na kuendelea hii ni kutokana na programu tutakayo tumia kufanya hatua hizi ndio inaitaji toleo hilo, basi baada ya kuhakikisha unatumia mfumo huo wa android download programu ya Private SMS & Call kutoka Play Store, unaweza kudownload programu hiyo maalum kwa kubofya hapo chini.

Advertisement

UPDATE : App hiyo imeondolewa kwenye soko la Play Store ila unaweza Kuipata Hapa

Baada ya kudownload na kuinstall programu hiyo fungua programu yako kisha endelea kwa kubofya Next mpaka utakapokuta mahali kwenye kipengele cha kuweka Password, kumbuka password hiyo ni muhimu kwani ndio itakayo tumiaka kufungua programu yako. Baada ya hapo weka barua pepe kisha bofya continue, hatua inayofuata utaulizwa kuweka programu hii kama default bofya ok kisha endelea mbele kwenye kuweka jina au majina ambayo unataka yasionekane kwenye simu yako.

Bofya “import from contact” kisha kwenye phonebook yako chagua jina au majina unayotaka meseji na call logs zake zisionekane pale mtu anapo piga simu au kutuma sms, baada ya hapo malizia kwa kuseti meseji ambayo itakuja pale mtu huyo anapo kutumia meseji, ukimaliza bofya save.

Kwa kufuata hatua hizo utakua umeweza kuficha sms au call logs za mtu fulani pale anapo piga simu au kutuma SMS. Kujua hatua zote angalia video hapo juu utapata kuelewa kwa urahisi zaidi. kumbuka kama una tatizo lolote kuhusu njia hii unaweza kuuliza swali lako kupitia Tanzania Tech Forums pia kama unataka kujifunza mambo mengi ya Teknolojia kwa njia ya video unaweza kutufuata kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.

10 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use