Jinsi ya Kucopy Maandishi Kwa Kutumia Kamera ya Simu

Utaweza kunakili (Copy) maandishi yoyote kwa kutumia kamera ya simu yako
Jinsi ya Kucopy Maandishi Kwa Kutumia Kamera ya Simu Jinsi ya Kucopy Maandishi Kwa Kutumia Kamera ya Simu

Kama wewe ni mmoja kati ya watu ambao hutumia muda mwingi kunakii vitu kutoka mahali popote na kuja kwenye simu yako basi njia hii itakusaidia sana. Kupitia simu yako ya Android au iOS utaweza kunakili maandishi yoyote yaliyopo sehemu yoyote kwa kutumia kamera ya simu yako.

Unacho takiwa kufanya kufuata hatua chache na ambazo nitakuelekeza hapo chini, kumbukua njia hii inaweza kufanya kazi kwenye simu yako kwa kutegemea kama simu yako inaweza kupakia programu ambayo nimekuwekea hapo chini. Basi bila kupoteza muda twende kwenye makala hii.

Advertisement

Unacho takiwa kufanya ni kupakua programu ya Google Lens kwenye simu yako ya Android au kama unatumia iOS basi pakua app ya Google, kutoka kwenye soko la App Store. Unaweza kupata programu hizo kwa kupitia link hapo chini, kumbuka kwa iOS unatakiwa kupakua app ya Google.

Download App Hapa Android

Unaweza kupata app hii pia kupitia mfumo wa iOS na moja kwa moja unaweza kudownload app kupitia link hapo chini.

Download App Hapa iOS

Baada ya kupakua app hizi hakikisha unafanya set up vizuri, ikiwa pamoja na kuunganisha app hizo na akaunti yako ya Google kisha endelea kwenye hatua zinazo fuata.

Fungua app hiyo kisha kwa pembeni upande wa kushoto utaona kitufe kimechorwa alama ya karatazi au mistari minne. Bofya hapo na moja kwa moja elekezea kamera ya simu yako kwenye maandishi unayotaka kunakili na bofya kitufe hicho katika na utaweza kuletewa maneno ya select to copy.

Unatakiwa kubofya sehemu ya copy to clipboard na moja kwa moja utaweza kupaste maandishi hayo sehemu yoyote ile inayotaka. Njia hii itakusaidia pale unapoona namba au kitu chochote mahali na huna muda wa kuandika unaweza kunakili kitu hicho kwa urahisi kwa kutumia njia hii.

Pia Google lensi inakuja na sehemu nyingine nyingi, kwa mfano unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutafsiri maneno yoyote yaliyopo kwenye picha kwa kutumia kamera ya simu yako. Unaweza kujifunza mengi zaidi kwa kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech na utapata kujifunza mambo mengi sana kwa upande wa teknolojia.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use