Niwazi kuwa AI inaendelea kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku, na kadri muda unavyo kwenda ni wazi kuwa ni lazima kujifunza kutumia AI ili kuendana na kasi ya teknolojia kwenye ulimwengu wa sasa.
Kuliona hili leo nimekuletea aina mpya ya AI yenye uwezo wa kubadilisha video yoyote ya YouTube kuwa podcast au kipindi cha mtandaoni. Kizuri ni kuwa ni bure kabisa kutumia mfumo huu wa AI.
Kwa ufupi kabisa mfumo huu unaitwa NotebookLM, ni mfumo ulio tengenezwa na kampuni ya Google na unakupa uwezao wa kufanya research au utafiti kwa urahisi kabisa. Kama wewe ni mmoja wa watafiti unaweza kutumia mfumo huu kuweka data zako na kisha utaweza kuchati nao kuweza kufahamu baadhi ya mambo yaliyopo kwenye data zako.
Unaweza kutumia mfumo huu kwa kuweka data za aina mbalimbali kama vile Link, YouTube Video, PDF, Google Slides, Google Docs, Video File, Audio File na vyanzo vingine mbalimbali. Kama unataka kujua jinsi mfumo huu unavyofanya kazi unaweza kutembelea Tanzania Tech English utajua zaidi.
Tengeneza Podcast kwa Kutumia NotebookLM
Kwa kuanza unatakiwa kuwa na akaunti ya Google kisha moja kwa moja tembelea link hapo chini na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa NotebookLM.
Baada ya hapo, kubali vigezo na masharti bofya sehemu ya Create ambayo ipo kati kati ya screen yako.
Baada ya kubofya sehemu ya create utaletewa ukurasa maalum ambao unatakiwa kuwa data zako, hapa ndipo unatakiwa kuweka Video, Link au Video yoyote kutoka YouTube. Chagua sehemu ya data unaotaka kisha bofya kuendelea.
Kwa mfano huu sisi tumechagua YouTube na moja kwa moja utaweka link ya Video unayotaka iwe podcast (Hata ya Kiswahili) kisha malizia kwa kubofya Insert.
Baada ya hapo moja kwa moja endelea kwa kuangalia upande wa juu kulia kuna sehemu ya Audio Overview kisha bofya Generate.
Baada ya hapo subiri kidogo kati ya dakika moja ama mbili kulingana na ukubwa wa data au urefu wa video uliyoweka. Baada ya hapo utaweza kuletewa Podcast ambayo unaweza kusikiliza au kudownload moja kwa moja na kuweka kwenye social media zako. Unaweza kusikiliza mfano hapo chini.
Kama unavyoweza kusikia hii podcast imetengenezwa na AI kwa asilimia 100, kutoka kwenye makala hii na ukweli ni kuwa uwezo wa mfumo huu wa AI ni wa kipekee na unaweza kudhani hawa ni watu halisi.
Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku, kwa urahisi zaidi unaweza kupakua app ya Tanzania Tech kupitia link hapo chini.