Ni kweli kwamba kuwa na simu yenye muonekano wa aina moja kwa muda mrefu inaboa sana, ni vizuri kubadilisha baadhi ya vitu kwenye simu yako ili uweze kuona simu yako kama ni mpya na pia kuna haja gani ya kutumia simu janja na wakati kwa muonekano simu yako inaonekana sio janja.?
Kuyaona hayo, ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea maujanja haya ambayo yataweza kukusaidia kubadilisha muandiko (Font) kwenye simu yako ya Android ya Tecno pamoja na Samsung. Kwa kuanza ni vyema kujua kuwa simu za Samsung au Tecno zinatofautina hivyo unaweza kuona sehemu hizi kwenye baadhi ya simu na kwenye simu nyingine usione, lakini pamoja na hayo unaweza kuuliza kwenye maoni hapo chini kama utakuwa hujaona sehemu hizi za kubadilisha muandiko.
Jinsi ya Kubadilisha Muandiko kwenye Simu za Tecno
Kama unatumia simu ya Tecno unaweza kubadilisha muonekano wa muandiko wa simu yako kwa kufuata hatua hizi chache. Unachltakiwa kufanya ni kuingia kwenye App ya Hi Theme, kisha chagua sehemu ya Font iliyoko chini upande wa kulia, Tafuta font unayo ipenda kisha bofya download na baada ya hapo bofya Appy.
Kama kwa namna yoyote App ya Hi Theme haipo kwenye simu yako basi unaweza kutumia App ya HiOS Launcher ambayo unaweza kuipata kupitia Play Store kwa kubofya link hapo chini.
Jinsi ya Kubadilisha Muandiko Kwenye Simu za Samsung
Kama unatumia simu ya Samsung natumaini unajua jinsi ya kubadilisha muandiko, lakini kama hujui ni rahisi sana. Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye sehemu ya Settings kisha ingia kwenye Display alafu tafuta sehemu iliyoandikwa Font au Font and screen zoom, baada ya hapo chini kidogo utaona baadhi ya miandiko michache iliyopo kwaajili ya kubadilisha chagua muandiko kisha malizia kwa kubofya OK.
Kama kwa namna yoyote unaona font zilizopo kwenye simu yako hazitoshi basi unaweza kupata font nyingine zaidi ya 500 ambazo ni special kwaajili ya simu za Samsung. Unaweza kudownload app kupitia link hapo chini kisha fuata hatua za awali hapo juu kubadilisha font kwenye simu yako ya Samsung.
Download Font Zaidi ya 500 Hapa
Kwa kufuata hatua hizi basi utakuwa umeweza kubadilisha muonekanao wa muandiko kwenye simu yako ya Android ya Tecno au simu za Samsung. Kama kwa namna yoyote utakuwa umekwama usiache kuuliza kupitia link hapo chini au kupitia Tanzania Tech Forums.
hi habr nimejarb na mm kubadilisha font lakn kwnye hi theme hkn font natumia spark 2 tecno
Samahani,nikidownload application kwenye cm yangu haifunguki inaniandikia.unfortunately …has stopped. Nifanyeje? Naomba msaada
Punguza vitu kwenye simu yako. Inawezekana memory imekuwa ndogo.
samahan mimi nikingia hainiletei front naona nitofaut kabisa natumia sim ya tecno pop 2 model tecno b1
Sumu yangu ni tecno w4 , nikiingia kwenye “SETTING—>DISPLAY—->FONTS nikitaka kudownload inakataa
Jaribu ku-restart