Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)

Hatua kwa hatua jinsi ya kuanza kutengeneza podcast kwa urahisi mtandaoni
Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%) Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)
©femmeactuelle.fr

Ni wazi kuwa kwa sasa watu hutumia mtandao zaidi kuliko kipindi cha nyuma, hii inatokana na kukuwa na kubadilika kwa njia za mawasiliano. Kuliona hili leo ningependa kuongea na wewe kuhusu podcast.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia podcast ni nini, ikiwa pamoja na njia bora na rahisi ya kuanza podcast bila kutumia gharama yoyote ikiwa pamoja na sababu kwanini uanze kutumia zaidi podcast kuliko njia nyingine za kufikisha maudhui.

Advertisement

Podcast ni nini

Je podcast ni nini.? Kama hili ni moja ya swali ambalo ulikuwa unajiuliza mara kwa mara basi majibu yake ni kama ifuatavyo. Podcast ni vipindi vya mtandao ambayo vipo kwenye mfumo wa sauti (MP3) na vipo kwenye mpangilio wa awamu.

Fikiria podcast kama vipindi vya redio lakini badala ya kuwepo kwenye redio vipindi hivi sasa vinakuwa kwenye Internet au kwenye mtandao.

Kwanini Uanzishe Podcast

Ukweli ni kwamba kadri teknolojia inavyozidi kukuwa ndipo wengi wetu tunavyo kuwa bize na shughuli za kila siku kiasi cha kukosa muda wa kufanya mambo ambayo kabla ya hapo tulikuwa tukifanya.

Kwa sasa ni wazi kuwa hata hapa unaposoma makala hii unaona kama una poteza muda mrefu, lakini swali ni kwamba ni watu wangapi wangesikiliza kama makala hii ingekuwa kwa sauti.?

Majibu ni wazi kuwa wengi wangesikiliza makala hii kutokana na kuwa na uwezo wa kusikiliza ukiwa popote na mahali popote, tofauti na makala za maandishi na video ambazo ni lazima kusoma au kuangalia ukiwa umetulia kama hapo ulipo.

Mfano wa Podcast

Kama unavyoweza kuona hapo chini, hiyo ndio sehemu tu ya podcast kutoka Tanzania Tech, sehemu ambayo itakuwa inakuletea habari mbalimbali za teknolojia na maujanja mbalimbali kwa njia ya sauti.

Mfano wa Podcast

Jinsi ya Kuanzisha Podcast

Sasa baada ya kusema hayo yote sasa twende kwenye kiini cha makala hii ambapo nita kuonyesha jinsi ya kuanzisha post cast yako kwa urahisi na haraka bila gharama yoyote.

Sasa hatua ya kwanza hakikisha unayo Internet kwenye simu yako kisha moja kwa moja nenda kwenye soko la Play Store au App Store na pakua app ya Anchor.

Unaweza kupakua App kupitia link hapo chini, kama unatumia Android chagua link ya Android, pia kama unatumia iOS chagua link ya iOS. Baada ya kudownload endelea kwenye maelezo hapo chini.

Download Hapa Android

Download Hapa iOS

Baada ya kudownload app hii kwenye simu yako, moja kwa moja fungua na kisha login kwa kutumia akaunti yako ya Google. Pia unaweza kutumia njia ya barua pepe kama unataka.

Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)

Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye uwanja wa kuanza kurekodi podcast zako, hatua inayo fuatia unatakiwa kubofya sehemu ya jumlisha iliyopo chini katikati.

Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)

Baada ya kubofya sehemu ya jumlisha kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu, moja kwa moja ruhusu app hii kutumia Mic ya simu yako na endelea kwa kubofya kitufe cha Mic na anza kuongea huku ukirekodi podcast yako.

Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)

Kupitia app hii utaweza kuedit podcast yako kwa urahisi, pia utaweza kupata nyimbo za bure za kutumia kwenye podcast yako kwa urahisi kwa kubofya sehemu ya sounds.

Baada ya kumaliza kurekodi unaweza kushare podcast yako kupitia mitandao ya Spotify, Google Podcast na mitandao mingine mikubwa ya podcast bila kutoka ndani ya app hii. App hii inamilikiwa na Spotify hivyo tegemea upatikanaji bora wa kipindi chako kupitia podcast yako hiyo.

Kwa kufanya hatua hizo natumaini unaweza sasa kutengeneza podcast yako ya kwanza bure bila kutumia gharama yoyote. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kujiunga nasi kupitia mtandao wa YouTube ambapo tunajifunza zaidi kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use