Hivi ulishawahi kujiuliza tovuti ya facebook.com ilikuaje ilipoanzishwa siku ya kwanza..? au ulisha wahi kujiuliza tovuti ya millardayo.com ilikuwaje ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza kabla tovuti hiyo haijawa maarufu..?
Kama umekuwa ukijiuliza maswali hayo basi pengine makala hii ni sahihi kwako, kupitia makala hii nitashare na wewe jinsi ya kuangalia muonekano wa tovuti yoyote ilipo anzishwa kwa mara ya kwanza ilikuwaje.
Njia hii ni rahisi na haitaji muda mrefu hivyo moja kwa moja twende nikushirikishe njia hii, kumbuka unaweza kuangalia tovuti yoyote ilivyokuwa hakikisha tu unajua domain ya tovuti hiyo.
Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya wayback machine, unaweza kutembelea tovuti hiyo kwa kubofya hapo chini.
Baada ya kuingia kwenye tovuti hiyo sasa kwenye sehemu ya kuandika andika jina la domain yoyote, kwa mfano unaweza kuandika millardayo.com au tanzaniatech.one au domain yoyote unayotaka kuangalia.
Baada ya hapo bofya sehemu ya Browse History, kisha subiri ukurasa huo upakie data na moja kwa moja utaweza kuona muonekano kama huo hapo chini.
Sasa kupitia sehemu hiyo yenye mawimbi pamoja na mwaka unaweza ku-slide kwa kwenda kulia na moja kwa moja utaweza kuona sehemu hiyo ikisoge na miaka ikibadilika, moja kwa moja chagua mwaka ambapo unaona mawimbi yalipo anzia na bofya hapo moja kwa moja.
Baada ya hapo sasa chagua tarehe ya kwanza ya ambapo unaona imezungushiwa duara. Baada ya hapo utaweza kuona imetokea tarehe na saa kwenye chumba maalum, bofya sehemu hiyo moja kwa moja.
Baada ya hapo sasa utaweza kuona muonekano wa tovuti hiyo ilivyokuwa kulingana na muda ulio chagua, unaweza kuona kila kitu ikiwa pamoja na kujaribu baadhi ya page zilizopo kwenye monekano wa tovuti hiyo wa zamani.
Kama unavyoweza kuona hivi ndivyo tovuti ya millardayo.com ilivyokuwa mwaka 2012, unaweza kuona kila kitu ikiwa pamoja na kusoma habari zilizokuwa kwenye tovuti hiyo kwa mara ya kwanza.
Mapaka hapo natumaini utakuwa umeweza kuangalia muonekano wa tovuti yoyote ilipo tengenezwa kwa mara ya kwanza. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza video za mitandao ya kijamii kwa urahisi bila kuwa na ujuzi.
Kama unataka kujifunza kwa vitendo hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube hapa na uhakika utaweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa pamoja na njia mbalimbali za kutengeneza pesa mtandaoni kwa urahisi na haraka.