Ni kweli kwamba hivi sasa usalama wa mtandao umekuwa ni kitu kigumu sana, imekuwa sio rahisi kuwa salama mtandao kama utakuwa huna utaratibu wa kutafuta njia mpya za kujiweka salama hasa kama unategemea mtandao kufanya mambo yako ya muhimu.
Kuliona hilo leo Tanzania Tech tunakeletea njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia kuweza kujua kama password unayo tumia ni salama kuendelea kutumia mtandaoni. Njia hii ni rahisi na inaweza kusaidia mtu yoyote anayetumia simu ya android.
Kwa kuanza ni muhimu kujua kuwa njia hii itakusaidia kila mara ambapo utakuwa unataka kuweka password kwenye akaunti yako yoyote, utaweza kupata ujumbe ambao utakutaarifu kama password hiyo ni salama au sio salama. Basi kwa kusema hayo moja kwa moja twende kwenye njia hii.
Kwa kuanza unatakiwa kuwa na kivinjari cha Google Chrome, simu nyingi za Android zinakuja na kivinjari hichi basi moja kwa moja kwa moja fungua kivinjari hicho na hakikisha una update kupitia Play Store. Baada ya hapo endelea kwenye hatua hizi.
Kwa kuanza fungua kivinjari au browser yako ya Google Chrome, kisha boffa vitufe vitatu vilivyopo upande wa kulia juu kisha chagua Settings.
Baada ya hapo moja kwa moja ingia kwenye sehemu ya Settings ya kivinjari cha Chrome, kisha moja kwa moja utaweza kuona Menu mpya ya ‘Safety Check’.
Baada ya hapo bofya sehemu hiyo na utaweza kuona sehemu nyingine ndani za Updates, Passwords, na Safe Browsing.
Baada ya hapo sasa bofya sehemu ya Check now na moja kwa moja utaweza kuona sehemu hii ikiangalia password ambazo zipo kwa muda huo. Kwa sababu ndio mara yako ya kwanza kutumia sehemu hii utaweza kuona kuwa sehemu hii bado haijapata password yoyote.
Kuanzia sasa sehemu hii itakua ina angalia password zako zote kama ni salama na utaletewa taarifa pale ambapo password yako itakuwa sio salama au imedukuliwa kwa namna yoyote.
Mpaka hapo utakuwa umemaliza kuwasha sehemu hii ambayo na hakika itakusaidia sana kama wewe ni mtumiaji wa mitandao mbalimbali mara kwa mara. Kumbuka sehemu hii inaweza kuangalia password zako pale tu utakapo kuwa unatumia kivinjari cha Google Chrome na sio vinginevyo.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kuzuia akaunti zako za mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Instagram kudukuliwa au kuwa hacked. Pia hakikisha una tengeneza password imara na isiyo dukuliwa kwa kusoma sheria za password hapa.