Wote tunajua internet au mtandao unaweza kuwa sehemu nzuri sana, lakini pia mtandao unaweza kuwa sehemu mbaya sana na kwa namna yoyote ile kama umefikia hatua unataka kujifuta kabisa mtandaoni basi hii ndio ya kufanya.
Huko swiden wataalamu wa kwenye mtandao wameweza kutengeneza programu yenye uwezo wa kufuta kila kitu kwenye mtandao kinachohusiana na wewe, hivyo kama unataka kufuta kila kitu chako unaweza kuingia kwenye tovuti hiyo kwa kubofya kwenye kitufe hapo chini kisha bofya Get started.
Baada ya kuingia kwenye tovuti hiyo jisajili kwa kutumia akaunti yako ya Google ambayo unataka ifutwe, maana yake ni kwamba kila kitu ambacho uliwahi kujisajili kwa kutumia barua pepe hiyo kitafutwa moja kwa moja yaani mpaka hiyo akaunti ya Google uliyotumia itafutwa moja kwa moja. Programu hii inatafuta chocote kile mtandaoni chenye email yako na kufutwa moja kwa moja.
Hivyo kama ulikuwa sio maarufu zamani na sasa umekuwa maarufu na unataka kufuta kila kitu cha zamani usiwe na wasiwasi cha muhimu ingia kwenye tovuti hii kisha bofya kitufe hapo juu kisha jaza email yako ya gmail kisha subiri kwa muda kisha utaona kila kitu kuhusu wewe kimefutwa. Kumbuka tu kuwa inawezekana kila kitu kisifutike kwa muda huo hivyo endelea kujaribu kadri muda unavyokwenda programu hiyo itazidi kujua kila kitu kilichopo mtandaoni kwa jina lako.
Kizuri ni kwamba unaweza kuchagua ni kitu gani cha kuacha na kitu gani cha kufuta hivyo nadhani hii ni kitu nzuri sana kwako…. kama umeipenda basi toa maoni yako hapo chini, pia kwa wadukuaji hii haitafanya kazi kwenu sababu hakuna mahali pa kujiandikisha zaidi ya kutumia akaunti yako binafsi.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video