Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Unataka Kuwa Mtaalamu wa Kuchora Tumia App ya SketchAR

Kama umekua ukipenda kujifunza kuchora basi jaribu app hii
Jifunze kuchora SketchAR Jifunze kuchora SketchAR

Kwenye ulimwengu wa sasa wa Teknolojia ni wazi kuwa mambo mengi sana yanafanyika kwa kutumia simu zetu za mkononi, ndio maana wataalamu kutoka kampuni SketchAR wanakuletea njia rahisi ya kujifunza kuchora kupitia simu yako ya mkononi.

Ni kweli kuwa kwa watu wengine kuchora ni kipaji lakini kama wewe ni kama mimi na kuchora kwako ni mthiani basi jaribu App hii mpya ya SketchAR. App hii inakupa uwezo wa kipekee kuweza kujifunza kuchora na ni rahisi sana kuitumia na huitaji ujuzi wowote zaidi ya kuwa na smartphone yako.

Advertisement

Kwa kutumia mfumo wa AR au Augmented Reality, App hii itakusaidia kuweza kuchora kwenye karatasi kwa kufuata hatua chache, Kwanza unachotakiwa kufanya ni kuchora vidoti vya duara kwenye karatasi yako kisha chukua simu yako na washa App ya SketchAR kisha chagua mchoro na nyooshea kamera yako kwenye karatasi zenye vidoti hivyo vya duara.

Kitakacho tokea ndani ya App hiyo kutatokea mchoro ambao utakuwa juu ya karatasi yako, mchoro huo utaonekana ndani ya kioo cha simu yako kisha unatakiwa kufuatiliza vipengele kwa vipengele jinsi App hiyo itakavyo kuwa ikikupa maelekezo. Njia hii ni rahisi na unaweza kujifunza kuchora kwa urahisi kwa kufanya mazoezi ya kila siku.

App hii inapatikana kwenye mifumo yote ya Android pamoja na iOS na unaweza kudownload sasa na kuanza kujifunza kuchora kwa kutumia simu yako. Bofya hapa chini kudownload kulingana na aina ya mfumo wa simu unayotumia.

  • SketchAR – Mfumo wa Android
  • SketchAR – Mfumo wa iOS

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use