Wakati kampuni za infinix na TECNO zikiwa tayari zimemaliza mwaka kwa simu zao zilizotoka hivi karibuni, kampuni ya Samsung yenyewe inajiandaa kumalizia mwaka na simu mpya ya Galaxy A51.
Kwa mujibu wa tovuti ya Sammobile,, Samsung inategemea kufanya tamasha la uzinduzi wa simu zake mpya ambazo zinategemewa kufunga mwaka 2019 na kuanza mwaka 2020. Kwa mujibu wa ripoti hizo Galaxy A51 na simu nyingine zinategemewa kuzinduliwa tarehe 12/12/2019 huko nchini Vietnam.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, kampuni ya Samsung imekuja na muonekano mpya kabisa wa simu zake za Galaxy A kwa mwaka 2020, simu hizi sasa zinakuja na kamera zaidi ya mbili ambazo zina muonekano wa pekee pamoja uwezo mkubwa. Galaxy A51 inasemkana kuja na kamera nne kwa nyumba huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48, Megapixel 12 na nyingine mbili za mwisho zikiwa na Megapixel 5 kila moja.
Mbali na hayo, Galaxy A51 inasemekana kuja na kioo cha AMOLED chenye ukubwa wa inch 6.5, kioo ambacho kina kuja na tundu dogo la kamera ya mbele ambayo inakuja na uwezo wa Megapixel 32. Hata hivyo simu nzima ya Galaxy A51 inaendeshwa na processor ya Exynos 9611 chipset, ikiwa inasaidiwa na RAM ya kati ya GB 4 au GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani kati ya GB 64 na GB 128. Uhifadhi huo unaweza kuongezwa kwa kutumia MicroSD Card.
Galaxy A51 inasemekana kupewa nguvu na battery yenye uwezo wa 4,000 mAh ambayo pia inakuja na teknolojia ya Fast Charging (15W charging) ambapo unaweza kuchaji simu hii hadi asilimia 50 ndani ya nusu saa.
Kwa taarifa zaidi hakikisha una ungana nasi tarehe 12/12/2019 siku ya alhamisi, tutakuwa mubashara kabisa tukikuletea matangazo ya moja kwa moja kuhusu uzinduzi wa simu hii mpya kutoka Samsung.