Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Je Unatumia iPhone Iliyovunjika Kioo? Soma Hii

Je Unatumia iPhone Iliyovunjika Kioo? Soma Hii Je Unatumia iPhone Iliyovunjika Kioo? Soma Hii

Je una smartphome ya iPhone iliyovunjika kioo? Basi usiwe na wasiwasi, sasa unaweza ukabadilisha iPhone yako na kupewa kiwango cha pesa, hili linawezekana ukiwa kwenye duka lolote la Apple Orignal imeripotiwa na vyanzo mbalimbali vya habari.

Huduma ya Apple iitwayo “Reuse and Recycling” ilikua ikitumika kwa kubadilisha model za zamani ambazo hazijaharibika za iPhone kwa kiwango cha kawaida cha pesa.

Advertisement

Mabadiliko mapya ya huduma hii yanaeleza kuwa sasa unaweza kubadilisha simu za iPhone  5s, iPhone  6 na iPhone  6 plus ambazo zinamatatizo ya kioo, vibonyezo, kamera pamoja na simu za iPhone  za zamani, imeripotiwa na blog ya 9To5Mac blogblog hiyo inasema uharibifu huo unatakiwa kuwa na sababu za msingi.

Kiwango cha pesa unacho pewa kwa kubadilisha simu yako kinategemeana na aina ya model ya simu uliyonayo, lakini repoti zinasema mtumiaji ategemee kiasi cha dollar za kimarekani $50 kwa iPhone 5c, $200 kwa iPhone 6 na $250 kwa iPhone 6 plus.

Kampuni ya Apple hivi karibuni imekuwa na wasiwasi na uuzaji wa simu zake. Kampuni hiyo kubwa ya simu marekani imekuwa na matumaini ya kufanya huduma hii ya kubadilisha simu kutumika watu wengi zaidi, ikiwa kampuni hiyo iko mbioni kutoa toleo jipya la iPhone 7 ndani ya mwaka huu.

Pia Blog ya 9To5Mac Blog inaseama Apple itatoa mashine za kuweka screen protector na iwapo mashine hizo zitakosea chochote wakati wa kuweka screen protector kwenye simu yako utapewa huduma ya bure ya kuwekewa screen protector hiyo yaani hutalipa tena. Kwa Tanzania hatujajua kama huduma hii ipo au kama inafanya kazi.

Shinda Vocha ya Shiling Elfu 10,000

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use