Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatimaye Sasa Unaweza Kujaribu Muonekano Mpya wa Gmail

Sasa unaweza kujaribu muonekano huo mpya kupitia kompyuta yako
Muonekano Mpya wa Gmail Muonekano Mpya wa Gmail

Hivi karibuni Google ilisemekana kufanya majaribio ya muonekano mpya wa Tovuti yake ya barua pepe ya Gmail, Sasa hivi leo Google imatangaza rasmi kuletea muonekano huo mpya na sasa unaweza kujaribu moja kwa moja kupitia kompyuta yako.

Muonekano huo mpya umeleta vitu mbalimbali vipya kwenye tovuti hiyo ikiwa pamoja na sehemu ya confidential mode ambapo utaweza kuweka tarehe maalum ya barua pepe kuonekana. Yaani unachokifanya ni kutuma link maalumu kwa unayetaka apate barua pape hiyo na pale mtu atakapo pata link hiyo ataweza kubofya na ataweza kusoma barua pepe hiyo ikiwa bado iko kwenye akaunti yako na pale muda ulio uweka utakapofika basi link hiyo itakuwa haifanyi kazi tena na mtu huyo hatoweza tena kusoma barua pepe hiyo.

Advertisement

Sehemu nyingine mpya ni Integrated rights management au (IRM), sehemu hii itakusaidia kuzuia baadhi ya barua pepe unazotaka zisiweze kutolewa nakala (printing), kushiriki na watu wengine (forwarding), kunakili (Copying) pamoja na kupakua barua pepe (Downloading).

Sehemu nyingine ni Two-factor authentication (2FA) ambayo itakuwezesha kuweka ulinzi wa ziada kwenye barua pepe uliyo mtumia mtu kwa kuongeza sehemu mpya ambayo itamlazimu aliyepokea barua pepe kuthibitisha kwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ili kuweza kufungua barua pepe hiyo.

Vilevile Katika muonekano huo mpya, Google inameleta sehemu mpya ya Reply ambayo itakuwa inafanya kazi kama ilivyo ile App au programu ya Reply kutoka Google. Sehemu hiyo mpya itakuwezesha kujibu barua pepe zako kwa kutumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence, kama vile jinsi programu hiyo ya Android ya Reply inavyo fanya kazi.

Mbali na hayo, Sehemu nyingine iliyofanyiwa mabadiliko ni pamoja na njia za kuchagua muonekano wa barua pepe zako ndani ya ukurasa wa Inbox. Muonekano huo mpya utakuja na sehemu mpya ambayo zitakuwezesha kuchagua aina ya muonekano unayotaka kulingana na wingi au uchache wa barua pepe zako ndani ya ukurasa wa inbox kwenye tovuti hiyo ya barua pepe ya Gmail.

Kutakuwa na aina ya kwanza ambayo ni Default, aina hii itakupa uwezo wa kuona vitu kama aina za viambatanisho (attachment) vilivyoko kwenye barua pepe kabla ya kuifungua, ikiwa pamoja na picha, slides, nyaraka (documents) pamoja na majedwali au (spreadsheets).

Aina nyingine itakuwa ni Comfortable, aina hii itakuwezesha kuondoa nembo zote zinazo onyesha aina za viambatanisho (attachment) na badala yake itabakiza pini maalumu inayotumika sasa kuonyesha kwamba barua pepe inakuja na kiambatanisho au (attachment).

Aina ya mwisho ya tatu itakuwa ni Compact, aina hii inafanana kabisa na aina ya pili ambayo ni Comfortable lakini utofauti wa aina hii upo kwenye mpangilio kwani aina hii itapunguza ukubwa wa urefu kutoka barua pepe moja hadi nyingine kwenye ukurasa wa inbox ndani ya tovuti hiyo ya barua pepe ya Gmail.

Kwa sasa unaweza kujaribu muonekano huu mpya kupitia kompyuta yako kwa kuingia kwenye tovuti ya barua pepe ya Gmail kisha kubofya kitufe cha Settings kilichopo juu upande wa kulia kisha bofya Try New Gmail na utaona muonekano huo mpya. Pia unaweza kurudisha muonekano wa zamani kama unataka kwa kubofya sehemu hiyo hiyo ya Settings kisha bofya Go back to Classic Gmail. Hata hivyo Google bado inaendelea kuboresha muonekano huo hivyo tegemea sehemu nyingine mpya kwenye siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use