Hivi karibuni, raisi wa urusi Vladimir Putin alishinda tena kwenye kinyanganyiro cha uraisi nchini humo na ili kuonyesha kufurahishwa na kitendo hicho, kampuni ya Caviar ambayo inahusika na kutengeneza vitu vya dhamani, imekuja na toleo la simu mpya ya iPhone X ya dhahabu maalum kwaajili ya kusherekea ushindi wa raisi huyo.
Tofauti na iPhone X ya kawaida kava la nyuma la simu hii limetengenezwa kwa kutumia dhahabu na badala ya kuweka alama ya kampuni ya Apple kwa nyuma, simu hii ina picha ya raisi urusi huku kwa chini kukiwa kuna alama ya umoja wa nchi hiyo na kwa chini kwenye ukingo wa simu hiyo kukiwa kumeandikwa maneno yenye maana ya “Tuko tayari kwa wakati mzuri ujao na tutafika huko”.
Simu hii imetengenezwa kwa dhahabu safi au (24K pure gold) simu hii imetengenezwa kwa vipuli tofauti vya dhahabu na kila kipuli kimetengenezewa namba maalum ya utambulishi na hii ni ili kuweza kuthibiti usalama na utofauti wake. Kampuni ya Caviar imesema kuwa, toleo la simu hiyo ni alama ya umoja na ushirikiano baina ya nchi hiyo kama inavyosema kauli ya raisi huyo.
Hata hivyo simu hizi zimetengenezwa maalum kwaajili ya watu 76 tu duniani hii ikiwa na maana kuwa simu hizi ni limited edition hii ikiwa na maana simu hizo zimetengenezwa 76 pekee. Sasa najua ulikuwa unasubiri kwa hamu kujua bei ya simu hii na ukweli ni kuwa simu hii sio bei rahisi kwani iPhone X ya dhahabu ya GB 64 itauzwa kwa dollar za marekani $4,600 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 10,400,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo.
Vilevile iPhone X ya Dhahabu ya GB 250 itakuja na bei ya dollar za marekani $5,000 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 11,300,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadlisha fedha vya siku ya leo. Simu hizi zote zinakuja na warranty ya mwaka mzima na kama unaitaka simu gharama za kusafirisha ulipo ni bure kabisa.
Mwaka jana kampuni hiyo ilitoa simu ya Nokia 3310 liyokuwa na alama ya muunganiko wa raisi wa marekani Donald Trump pamoja na raisi wa urusi Vladmir Putin, simu hiyo ilikuwa inauzwa kwa takribani shilingi za kitanzania Tsh 5,000,000.
Tivuti bora ya habari. I love it.