Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Galaxy S8 Vs iPhone X Simu Ipi ni Bora Zaidi..?

Je wew unadhani kwa majaribio haya ni simu gani bora kwako
iPhone na Galaxy S8 iPhone na Galaxy S8

Kwa kuanza napenda niweke wazi kuwa makala hii haijafadhiliwa na kampuni yoyote kati ya hizi, hivyo nitaenda kuangalia ubora wa simu hizi kwa haki na hii itakuwa kwa muibu wa video hivyo wapenzi wa Samsung au Apple tafadhali msichukieee…..

Bila kupoteza muda twende tukangalie hatua moja baada ya nyingine, kumbuka mwishoni wa makala hii utaweza kupata nafasi ya kupiga kura ni simu gani wewe ungependelea kutokana na makala hii, hivyo soma makala hii mpaka mwisho..

Advertisement

  • Ubora wa Kioo

Kwa upande wa kioo Galaxy S8 imetengenezwa kwa kutumia kioo cha Gorilla Glass 5 wakati  iPhone X hii imetengenezwa kwa kioo ambacho Apple inadai kuwa ni kioo kigumu kuliko vioo vyote kwenye ulimwengu huu wa Smartphone mhh sijui.!.. hebu angalia hii..

  • Uwezo wa Kuzuia Maji

Samsung Galaxy S8 inayo uwezo wa kuzuia maji (water resist), simu hii ina weza kukaa kwenye maji ya ujazo wa meter 1.5 kwa muda wa nusu saa hii ni kwa mujibu wa Samsung, uwezo wake huo umepimwa na kupewa alama 68 hii ni sawa na vipimo vya IP, au Ingress Protection vya IP68. Kwa upande wa iPhone X simu hii pia ina uwezo wa kuzuia maji huku ikiwa na uwezo wa kukaa kwenye maji ya meter 1 kwa muda wa dakika 20 au 25 na kwa mujibu wa vipimo vya ubora wa kuzuia maji na vumbi simu hii imepewa alama IP67.

  • Uwezo wa Kuimili Joto Kali

Kwa mtu ambaye unaishi sehemu kama Dar es salaam au Dodoma kwa hapa tanzania ni vizuri sana ujue kama simu yako inauwezo wa kuimili joto kali la sehemu hizi, kuna wakati watu unakuta wana lalamika kuwa kaweka simu mfukoni kwa muda mrefu na baadae unakuta simu imezima na inakuwa na joto sana, hii hutokana na simu kutokuwa na uwezo wa kuimili joto kali.

Je vipi kwa upande wa simu hizi za  Samsung Galaxy S8 na iPhone X, itakuwaje zikiwashwa moto kwa muda wa sekunde 15..?, Najua hii sio sawa na joto la eneo lolote lakini hii itakupa idea ni simu gani inauwezo wa kuimili joto kali zaidi.

  • Ubora wa Kamera

Kwa upande wa Galaxy S8 simu hii inakuja na kamera ya nyuma yenye megapixel 12 yenye teknolojia za F/1.7 autofocus pamoja na optical image stabilization. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya megapixel 8 yenye teknolojia za F/1.7 na autofocus.

Tukiangalia upande wa iPhone X simu hii inakuja na kamera mbili za nyumba zenye uwezo wa megapixel 12 wide-angle yenye teknolojia ya f/1.8 aperture na nyingine yenye Megapixel 12 f/1.8 yenye teknolojia ya f/2.8 aperture, optical zoom up to 2x pamoja na optical image stabilization, Kamera ya mbele ina uwezo wa Megapixel 7 yenye teknolojia ya f/2.2 aperture.

  • Uwezo wa Kujaa Chaji Haraka

Wote tunajua kuwa Galaxy S8 inakuja na uwezo wa kujaa chaji kwa haraka (Fast Charging) ikiwa inauwezo wa kujaa chaji asilimia 50 kwa nusu saa. Vilevile kwa upande wa iphone x simu hii pia inakuja na uwezo wa fast charging huku ikiwa na uwezo wa kujaa chaji kwa asilimia 50 kwa muda wa nusu saa, lakini je ni kweli..? Angalia video hii. (Angalia muda wa iPhone X na Samsung S8)

Natumaini mpaka hapo utakuwa umepata idea ni simu gani ambayo pengine itakuwa bora kwako, sasa tuambie kwa kuchagua kati ya Galaxy S8 na iPhone X unadhani simu gani ni bora kwako..? kumbuka matokeo ya kura hizi yanaweza kukusaidia wewe au hata jirani yako kujua ni simu gani anunue kati ya hizi mbili.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

3 comments
  1. Nimependa jinsi mnavyotoa review zenu, mnajitahidi sana. Kwangu mm nimeipenda Galaxy S8 kwan iko so 2017 kuliko IPhone ten!!!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use