Kampuni ya Apple inatarajia kufanya mkutano wake jumatano ya wiki hii, ndani ya mkutano huo kampuni hiyo inatarajiwa kuzindua simu zake mpya tatu ambazo ndio simu mpya za apple kwa mwaka 2019.
Kama umekuwa msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech nadhani utakuwa umesha fanikiwa kujua kuhusu uzinduzi wa simu hizo mpya za iphone, lakini kama bado wewe ni mgeni hapa Tanzania Tech basi ni vyema nikujulishe kuwa hapa Tanzania Tech tulisha fanikiwa kupata muonekano wa simu hizo ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa hapo siku ya jumatano.
Simu zenyewe ni pamoja na matoleo mapya ya iPhone X, pamoja na toleo jipya la iPhone ambalo kwa mujibu wa tetesi inasemekana litakuwa ndio toleo la simu hizo la bei rahisi kwa mwaka huu. Hata hivyo kwa mujibu wa tetesi hizo kutoka tovuti za Macotakara na 9to5Mac matoleo hayo mapya ya iPhone X yanatarajiwa kupewa majina ya iPhone XS, iPhone XS Plus, pamoja na toleo hilo la bei rahisi ambalo litapewa jina la iPhone XC.
Mbali na hayo, tovuti ya 9to5Mac imeainisha kuwa simu hizo zitauzwa kwa bei ya dollar $699 sawa na Tsh 1,594,000 kwa iPhone ya bei nafuu ambayo ni iPhone XC, Dollar $900 sawa na Tsh 2,054,000 kwa iPhone XS, na dollar $1000 ambayo ni sawa na Tsh 2,282,000 kwa iPhone XS Plus.
Vilevile vile kwa mujibu wa tetesi nyingine kwenye mitandao mbalimbali, simu hizi mpya za iPhone zinatarajiwa kuja na rangi za red, white, pamoja na blue kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.
Kwa sasa ni hayo tu kuhusu ujio wa simu mpya kutoka kampuni ya Apple, Hakikisha upitwi na uzinduzi wa simu hizi kwani tutakuwa mubashara kabisa tukikuletea uzinduzi huo moja kwa moja kupitia hapa Tanzania Tech.