Mwaka unakimbilia mwishoni na wakati ikiwa zimabaki siku chache kufikia mwezi wa tisa tayari tetesi za simu mpya za iPhone zimesha anza kuzuka mtandaoni. Mpaka sasa tayari kuna tetesi nyingi sana za kuhusu muonekano wa simu hizo ikiwa pamoja na baadhi ya sifa ambazo ndio zinasemekana kuwa ndio sifa za simu hizo.
Sasa tukiachana na tetesi hizo ambazo hivi leo Tanzania Tech tumefanikiwa kupata muonekano ambao ndio muonekano halisi wa simu hizo mpya ambazo zinategemewa kuzinduliwa mwezi ujao huko nchini marekani. Tetesi hizi zinauhakika kwa asilimia kubwa kutokana na mahali ambapo tumefanikiwa kupata tetesi hizi hivyo ni matumaini yangu umejiandaa kuona simu yako ijayo.
Kwa kuanza nadhani umesoma kichwa cha habari kikisema SIMU ZA IPHONE hiyo ikimaanisha kuwa mwaka huu kampuni ya Apple inaenda kuzindua simu za iPhone zaidi ya moja. Simu zinazotarajiwa kuzinduliwa ni pamoja na iPhone X au iPhone 10, iPhone X Plus au iPhone 10 Plus pamoja na iPhone X Lite. Sasa hapa kwenye majina haya chanzo cha habari hizi kinasema bado hakuna uhakika kama simu hizi zitakuwa na majina hayo… anyway labda tuone muonekano wa simu hizi kwanza.
Kama unavyona kwenye picha hapo juu kutakuwa na simu tatu ambayo ya kwanza ni toleo la maboresho la iPhone X, ambalo litakuja na maboresho ya sifa za ndani na kutakuwa hakuna mabadiliko makubwa zaidi ya sifa za ndani pamoja na kuongezewa rangi moja ya Gold, yaani ni sawa na kusema kutakuwa na simu mpya ya iPhone X ya rangi ya Gold.
Simu nyingine ambayo hii itakuwa ni ingizo jipya itakuwa ni iPhone X Plus, simu hii itakuja na kioo kikubwa cha inch 6.5 chenye kutumia teknolojia ya OLED, vilevile inasemekana simu hiyo itakuja na battery kubwa zaidi ni sawa na kusema simu hii itakuja na kila kitu kikubwa pengine usishangae pia kusikia simu hii ikija na ukubwa wa ndani mkubwa zaidi kuliko matoleo mengine. Mbali na ukubwa simu hii pia inasemekana kuwa ndio itakuwa ya bei ghali zaidi.
Toleo lingine ambalo ndio toleo la mwisho ni iPhone X Lite (Bado jina halija thibitishwa), simu hiyo inatarajiwa kuwa na kioo cha inch 6.1 ambacho kinatumia teknolojia ya LCD tofauti na simu zilizotangulia. Kitu kingine cha tofauti kwenye simu hii ni kuwa, inategemewa kuwa na kamera moja kwa nyuma na sio mbili kama zilivyo simu zilizo tangulia. Vilevile simu hii ndio inatarajiwa kuja na rangi nyingi tofauti na pia ndio toleo la bei rahisi la simu hizo mpya za iPhone 2018 – 2019.
Na hizo ndio simu mpya za iPhone ambazo ndio zinatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao na kampuni ya Apple huko nchini marekani. Kuhusu sifa kamili za simu hizi bado hazija julikana na bado hatujaweza kupata chanzo ambacho kinaweza kutupa sifa ambazo pengine ni sahihi kuhusu simu hizi mpya. Mabadiliko ni kama hayo niliyo kuambia hapo juu ila pia inasemekana kuwa simu mbili za iPhone X na iPhone X Plus zitakuja na teknolojia mpya ya (Face ID 2.0) wakati iPhone X Lite yenyewe itakuja na teknolojia ya (Face ID 1.0).
Kuhusu makadirio ya bei, tegemea kupata simu za iPhone X kwa bei ile ile ya takribani Tsh 2,500,000 hadi 3,500,000 na iPhone X Plus tegemea kuipata kwa bei ghali zaidi kuanzia Tsh 4,000,000 hadi 4,500,000 wakati toleo la iPhone X Lite tegemea kuipata kwa madirio kuanzia Tsh 1,500,000 hadi Tsh 2,000,000. Kumbuka bei hizi ni kwa makadirio hivyo simu hizo zinaweza kuuzwa kwa bei ghali zaidi.
Na huo ndio muonekano wa simu hizo mpya za iPhone, kwa taarifa zaidi kuhusu simu hizo endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia jiandae na uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9 hapo kesho tutakuwa mubashara kabisa tukikuletea matangazo ya moja kwa moja.
hizo simu bei gani..?.Huawei