Kama wewe ni mtumiaji wa bidhaa za Apple kama iPhone 5, iPhone 4S, iPad mini, iPad 2, na iPad 3rd generation basi unatakiwa kuchukua hatua za haraka sana kabla kifaa chako hakija acha kufanya kazi vizuri kwenye App muhimu.
Kwa mujibu wa tovuti ya CNBC, kampuni ya Apple imetangaza kuanzia tarehe moja mwezi huu ni muhimu watumiaji wa vifaa hivyo kufanya update ya toleo jipya la iOS 10.3.4, toleo ambalo ni muhimu sana kwenye simu hizo ili kuendelea kufanya kazi vizuri.
Kwa mujibu wa Apple, bila ku-install update hizo vifaa hivyo ikiwa pamoja na iPhone 5 zilizotoka kuanzia mwaka 2012 zote zitashindwa kufanya kazi vizuri hasa app za muhimu kama App Store, iCloud, email, web, na huduma nyingine ambazo zinatumia mfumo wa GPS pamoja na saa na tarehe.
Hata hivyo Apple imaendika kuwa, update hizo ni muhimu kutokana na mfumo wa GPS jinsi unavyofanya kazi kwani huesabu wiki kwa kutumia kipimo kina choitwa ten-bit parameter. Kipimo hicho kina hesabu wiki kuanzia wiki sifuri na kuanza upya kila inapofika wiki ya 1,024. Kwa mujibu wa tovuti ya The verge, wiki ya kwanza ilianza kuhesabiwa mwaka 1980 na hivyo kipimo hicho kitakuwa kina anza upya ilipofika mwaka 1999.
Hii ina maana kuwa, kipimo hicho kilianza kuhesabu tena kuanzia mwaka 1999 na hadi ilipofika tarehe 6 ya mwezi wa nne 2019 kipimo hicho kilikamilisha mzunguko wa wiki 1,024 na kuanza upya kuanzia tarehe hiyo. Sasa kila mzunguko unapo anza simu ambazo hazina toleo jipya la mfumo wa uendeshaji hushindwa kusoma muda vizuri na hivyo kushindwa kutumia GPS kwani GPS hutegemea sana muda kuweza kufanya kazi vizuri. Unaweza kusoma hapa kujua zaidi kuhusu hili.
Kwa mujibu wa The verge, tatizo la kuanza upya kwa kipimo hicho linaweza lisionekane moja kwa moja ile tarehe ya kuanza mzunguko upya, bali inaweza kuwa baadae sana baada ya tarehe hiyo kupita. Hii ndio maana vifaa hivi vya Apple vimekuja kuathirika sasa, Kwa mujibu wa Apple tatizo kwenye simu hizo linaweza kuanza kuonekana kuanzia tarehe 3 Novemba mwaka 2019 (Siku ya Jana kwa marekani) kuanzia saa 12:00 am ambayo ni sawa na saa tisa kamili za usiku siku ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.
Kama wewe unatumia simu ya iPhone 5, kitu cha muhimu ni kuhakikisha una angalia toleo hilo jipya kwani bila kufanya hivyo unaweza kushindwa kutumia simu yako vizuri. Kama unataka kujua kwa undani zaidi unaweza kusoma hapa taarifa kamili ya Apple kwa watumiaji wa simu hizo.
Kama unataka kuangalia update kwenye simu yako unaweza kufuata hatua hizi fupi, Fungua app ya Settings, kisha bofya General, kisha chagua About kisha angalia toleo la mfumo wa iOS hakikisha mfumo huo ni iOS 10.3.4. Bila hivyo bofya sehemu ya update kuangalia update.
Kwa habari zaidi za teknolojia, pamoja na kujifunza maujanja mbalimbali hakikisha una pakuwa app ya Tanzania Tech kupitia soko la Play Store.