Tunapokaribia kumaliza mwaka 2018 na kuingia mwaka 2019 ukweli ni kwamba yapo mambo mengi tunayo yawazia ambayo yamepita lakini pia yapo tunayoyawazia yanayo kuju huku tukijiuliza yapi yatafaa kwenye mwaka au miaka inayokuja.
Kwenye ulimwengu wa teknolojia hasa simu janja za mkononi tumeona simu nyingi mpya mwaka huu 2016 na hata zingine zikiendelea kutoka mwezi huu wa mwisho wa December, lakini bado swali linabaki Je ni simu gani ambayo unatakiwa kuanza nayo mwaka 2019.
- Simu ya Android
Ili kutimiza lengo la simu gani utakayo anza nayo mwaka ni vyema kujua ni sifa gani na uwezo gani unahitaji katika simu unayohitaji na unaposema simu za android ni simu zinazojulikana sana kwa kukupa uwezo wa kufanya zaidi karibia kwenye kila kitu. Kwa wale wanaotumia android nadhani watakua wanajua nachosema hapa.
Kwa mfano kwenye android unaweza kubadilisha kabisa muonekano wa simu yako kwa kuweka programu au App fulani ambayo itakupa uwezo wa kubadilisha muonekano mzima wa simu yako. Yani kwa kuweka programu tu!!! utawezakuona simu yako kama mpya kabisa.
Hivyo basi kama unataka simu ya kukupa uwezo wa kufanya zaidi Android ni simu yako, sababu ni nyingi sana kama vile upatikanaji wa vifaa ni mrahisi sana, uwezo wa simu yako kufanya zaidi pia ni mkubwa sana, hayo na mengine mengi yanafanya simu za android kuwa nyepesi kutumia na rahisi kuwa nayo. Mwisho niseme tu kuwa kama unataka zaidi kwenye upande wa simu janja za mkonini (smartphone) basi nivyema kutumia simu za Android.
- Simu ya iOS
Tunaposema iOS hapa namanisha simu zote kutoka kampuni ya Apple, ukweli ni kwamba Apple ni kampuni ambayo imekua ikitengeneza inachokitaka na sio wateja wanachotaka, hii sio mbaya kwani kwa kufanya hivi inakupa hamu ya kutaka kujua kampuni hiyo itakuja na nini kwenye toleo lake linalokuja.
kwa kufanya hivi iOS imekua ni simu ambazo ziko (professional) maalum sana kwani kwa wanaotumia simu hii watakua wanajua kuwa, ukiwa unatumia iOS ina maana kuwa unatumia simu ambayo iko jinsi ilivyo, hutoweza kubadilisha kama wewe unavyotaka zaidi ya kile ulichowekewa kama uliwekewa uwezo fulani basi ndio huo huo hutoweza kubadilisha.
Simu hii imekua ikitumiwa na watu wengi wasiopenda kuumiza kichwa, vilevile simu hii hutumiwa na watu wengi ambao wanaridhika haraka kwenye upande wa simu walizonazo, ndio maana watu wengi wanaotumia simu hizi hudumu nazo kwa mda mrefu mpaka pale zitakapo haribika au kupotea. Hivyo mwisho ni kwamba kama unataka kununua simu isio na usumbufu na isiyo na uwezo zaidi ya ule unaotaka basi iOS ni simu bora sana kwako.
Bila shaka utakuwa umepata mwanga wa simu gani unayotakiwa kununua unapoanza mwaka 2019, nivyema kukumbuka kuwa simu bora ni ile inayofanya kila kitu unachotaka.