Kampuni ya Apple hivi karibuni imetangaza ujio wa mfumo wake mpya wa iOS 14.5, pamoja na mfumo mpya wa Watch OS 7.5. Mfumo huu mpya unakuja na maboresho mengi ambayo baadhi yake tutaenda kuangalia kwenye makala hii.
Kama unataka kujua mabadiliko yote yaliyopo kwenye mfumo huu mpya wa iOS 14.5 na Watch OS 7.5 unaweza kuangalia video hapo chini na utaweza kujua mabadiliko yote hatua kwa hatua.
TABLE OF CONTENTS
Unlock iPhone kwa Kutumia Apple Watch
Kwa kuanza baadhi ya mabadiliko ambayo ni makubwa ni pamoja na kufungua au ku-unlock iPhone yako kwa kutumia Apple Watch, sehemu hii itakuwa inafanya kazi endapo utakuwa umevaa mask pekee. Baada ya kusasisha toleo jipya unaweza kupata sehemu hiii kupitia Settings > Face ID & Passcode unaweza kuwasha moja kwa moja kupitia sehemu mpya ya Unlock with Apple Watch.
Baada ya kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja ukiwa umevaa mask angalia simu yako na moja kwa moja ukiwa umevaa Apple Watch yako na utaona Simu yako ikikuruhusu kufunguka kwa kutumia Apple Watch, utaona ujumbe maalum kupitia Apple Watch yako.
Pia unaweza kulock simu yako kwa kutumia Apple Watch lakini wakati wa kuja kufungua simu yako itakulazimu kuweka passcode kabla ya kutumia simu yako. Ili kupata sehemu hii pia saa yako ya Apple Watch inatakiwa kuwa na mfumo mpya wa Watch OS 7.4.
Emoji Mpya
Mabadiliko mengine kwenye mfumo huu wa iOS 14.5 ni pamoja na aina mpya za emoji ambazo sasa pia utaweza kuchagua rangi ya ngozi kwenye emoji za wapenzi au Couple. Hapo awali ulikuwa unaweza kuchagua rangi ya ngozi kwenye emoji ambazo ni za mtu mmoja mmoja pekee, sasa utaweza kuchagua rangi kwenye emoji za wapenzi kwa kushikilia emoji husika.
Mbali na hayo pia kuna emoji mpya kabisa ambazo zimeongezwa kwenye mfumo huo na unaweza kuzitumia moja kwa moja baada ya kusasisha au ku-update.
Maboresho Kwenye App ya “Find My”
Hivi karibuni Apple ilizindua Air Tag, kifaa kipya kabisa ambacho kinaweza kukusaidia kupata vitu vyako pale vinapo potea, sehemu hii hufanya kazi sambamba na app ya Find My ambapo sasa sehemu ya Items imeongezwa kwaajili ya kuwa vifaa vyako kulingana na kifaa cha Air Tag.
Sauti Mpya Kupitia Siri (Siri Voices)
Kwa watumiaji wa Siri, Apple imeongeza lafudhi mpya kupitia kwenye programu ya Siri na sasa utaweza kusikia siri ikiongea kwa lafudhi mbili mpya za kimarekani. Unaweza kupata lafudhi hizo kwa kuingia kwenye Settings > Siri & Search > Siri Voice, kisha chagua American, chini yake utaona lafudhi zikiwa nne tofaut na awali ambapo zilikuwa mbili pekee, Voice 2 na Voice 3 ndio mpya.
Pia kwa wale watumiaji wa mara ya kwanza wa Siri sasa utaweza kuchagua lafudhi na sio kama awali ambapo ilikuwa ni lazima siri itumie sauti ya kike pekee.
Pia sasa unaweza kupokea simu na kukata kwa kutumia siri bila kusema “Hey Siri”, sasa utaweza kukata simu kwa kusema neno moja kwa mfano “Answer it” kupokea simu au “Cancel it” kukata simu. Hii itakuwa ina fanyakazi kama umevaa headphone ambazo zina endana na Apple.
Wallpaper Mpya
Kupitia mfumo mpya wa iOS 14.5 Apple imeongeza wallpaper mbili mpya za purple ambapo sasa zina endana na toleo jipya la iPhone 12 ambalo linakuja na rangi inayo fanana. Unaweza kupakua wallpaper hizo mpya za iPhone kupitia link hapo chini.
Na hayo ndio baadhi ya mabadiliko makubwa ya mfumo mpya wa iOS 14.5 na mfumo wa Watch OS 7.4. Kama unataka kujua mabadiliko yote unaweza kuangalia video hapo chini kujua yote kuhusu mfumo wa iOS 14.5.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu mfumo wa iOS hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku. Kwa habari zaidi unaweza kusoma hapa kulingamisha mabadiliko ya iOS 14 na iOS 14.5.