Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Yote Mapya kwenye Mfumo Mpya wa iOS 12.2 (Download)

Download hapa mfumo mpya wa iOS 12.2 kwa ajili ya kifaa chako cha Apple
Fahamu Yote Mapya kwenye Mfumo Mpya wa iOS 12.2 (Download) Fahamu Yote Mapya kwenye Mfumo Mpya wa iOS 12.2 (Download)

Kama wewe ni mtumiaji wa simu zenye mfumo wa iOS basi lazima utakuwa unajua kuhusu mfumo mpya wa iOS 12.2, mfumo huu mpya kama ilivyokuwa kwenye iOS 12 unaweza kuinstall kwenye vifaa vyote vyenye kusupport mfumo wa awali wa iOS 12.

Kupitia kwenyemakala hii utaenda kujua yote mapya yaliyomo kwenye mfumo huo mpya wa iOS 12.2 pamoja na jinsi ya kuweza ku-install mfumo huu mpya kwenye kifaa chako cha Apple sasa hivi. Basi baada ya kusema hayo twende tuka angalie yote mapya kwenye mfumo huu mpya.

Advertisement

Apple News+

Kama ulisoma makala iliyopita basi lazima utakuwa unajua kuhusu Apple News Plus, huduma mpya ambayo itakupa uwezo wa kusoma makala na habari mbalimbali kutoka kwenye majarida zaidi ya 300 pamoja na tovuti mbalimbali. Kama nilivyo kwambia kwenye makala hiyo, App ya Apple News haipatikani kwa Tanzania ila unawea kuipata kwa kufuata maujanja niliyo kuwekea kwenye ukurasa huo.

Apple News+ inapatikana kwenye vifaa vyote vya Apple na itakuwa inapatikana kwa kulipia kwa mwezi kiasi cha dollar $9.99 ambayo ni sawa na Tsh 25,000 kwa mwezi. Unapo update mfumo huu mpya wa iOS 12 unaweza kupata app ya Apple News ikiwa na huduma ya Apple News+ ambayo utaweza kutumia bure kwa mwezi mmoja wa kwanza.

Aina Mpya za Animoji

Kwenye mfumo huu mpya wa iOS 12.2 unaweza kutumia aina mpya za Animoji ambazo zitakuwa zimeongezwa. Animoji hizo ni pamoja na Twiga, Samaki Papa, Nguruwe pori, pamoja na Bundi.

Fahamu Yote Mapya kwenye Mfumo Mpya wa iOS 12.2 (Download)

Mabadiliko Mengine Madogo

Mabadiliko mengine yaliyopo kwenye mfumo huu mpya wa iOS 12.2 ni ya kawaida na mabadiliko yenyewe ni pamoja na Marekebisho ya sehemu ya voice messages, mabadiliko ya kivinjari cha safari ambapo sasa kama website haina https itaandikwa Not Secure pamoja na mabadiliko mengine madogo ya sehemu ya ramani au Maps.

Jinsi ya Ku-update iPhone au iPad

Kwa sasa kama unataka ku-update kifaa chako unaweza kubofya sehemu ya Settings > General > kisha bofya > Software Update. Baada ya hapo utaweza kuona simu yako ikifauta update na kuanza kudownload moja kwa moja, hakikisha simu yako inayo chaji angalau asilimi 50.

Fahamu Yote Mapya kwenye Mfumo Mpya wa iOS 12.2 (Download)

Kama utashindwa ku-update kwa kutumia njia hii unaweza kutumia njia ya ku-update kwa kutumia iTune na hakikisha unao waya Orgnal wa kifaa chako. Unaweza kudownload mfumo kulingana na kifaa chako hapo chini.

Kama unataka kujua jinsi ya ku-update kwa kutumia njia hii unaweza kuangalia video kupitia hapa na utaweza kujua njia zote hatua kwa hatua.

Na hayo ndio yote mapya ambayo yapo kwenye mfumo huu mpya wa iOS 12.2 mfumo ambap umetoka rasmi hapo siku ya jana. Kwa taarifa zaidi kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu bidhaa za Apple hakikisha una tembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

2 comments
  1. mimi siyo maoni bali ni swali kwa nini ili ku apdate simu za iphone mara nyingi simu zinalazimisha mtu atumke Wifi huku simu za samsung zinapigwa apdate bila kuhitaji Wifi???
    ni njoa gani ya kifanya apdate bila Wifi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use