Inawezekana kwa namna moja ama nyingine hii ni mara yako ya kwanza kusikia app ya kuchati kutoka instagram inayoitwa direct, hii inatokana na kuwa app hii kwa namna moja ama nyingine ilikuwa haipatikani hapa Tanzania.
Lakini kama wewe ni msomaji wa Tanzania Tech, najua umeshawahi kujaribu app hii kwani kipindi cha nyuma tulishawahi kuonyesha jinsi ya kudownload app hiyo na kuinstall kwenye simu yako ya Android.
Sasa kama hukuweza kujaribu app hiyo kipindi hicho, ripoti mpya kutoka Instagram zinasema kuwa app hiyo imetangazwa kusitishwa na haitokuwa inaboreshwa tena na Instagram. Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya TechCrunch, instagram imesema inasitisha app hiyo na matumizi yote ya app hiyo yatarudisha kwenye sehemu ya DM ndani ya App ya Instagram.
Kama ulikuwa huijui app ya Direct, app hiyo ilikuwa inakupa urahisi wa kuchati na ndugu na jamaa ambao wapo kwenye mtandao wa Instagram huku pia ikikupa urahisi wa kuangalia Srories kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watu ulio wafuata.
Kwa sasa Facebook ipo kwenye mpango wa kuunganisha programu zake za Facebook, Instagram na WhatsApp ili kutoa urahisi kwa watumiaji kutumia programu hizo kwa urahisi pamoja na wafanya biashara kuweza kutangaza biashara zao kwa mapana zaidi.