Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode)

Sasa unaweza kuwasha dark mode kupitia app ya Instagram
Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode) Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao waliokua wanatamani kupata muonekano wa giza au dark mode kwenye programu yako ya Instagram basi sasa unaweza kufanya hivyo.

Mara baada ya kuweka sehemu ya Dark Mode kwenye WhatsApp, hatimaye hivi karibuni mtandao wa Instagram nao umeleta sehemu mpya ya kuwasha muonekano wa giza au dark mode.

Advertisement

Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode)

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, watumiaji wote wataweza kupata muonekano huo bila kujalisha aina ya simu unayo tumia. Njia hii ni tofauti na njia ambayo tulionyesha kipindi cha nyuma kwani njia ile ilikuwa ni lazima kuinstall programu ya ziada.

Kwa sasa huna haja ya kuinstal programu yoyote ya ziada kwani sasa utaweza kuwasha muonekano wa giza au dark mode moja kwa moja kupitia app ya Instagram. Unacho takiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo.

Jinsi ya Kuwasha Dark Mode Instagram

  1. Ingia kwenye ukurasa wako wa Instagram kisha bofya Menu iliyopo juu upande wa kulia, alafu chagua settings iliyopo mwisho wa ukurasa huo wa Menu.

Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode)

2. Kwenye ukurasa wa Settings, Chagua Theme iliyopo mwisho wa ukurasa wa Settings.

Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode)

3. Baada ya hapo chagua sehemu ya Dark kwenye ukurasa huo wa Theme. Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona Instagram yako imebadilika na kuwa na muonekano wa giza.

Instagram Yaleta Muonekano Mpya wa Giza (Dark Mode)

Njia hii inafanya kazi kwenye simu zote za Android na iOS na unaweza kupata sehemu hii kwa urahisi kabisa kupitia app ya Instagram. Kama kwa namna yoyote ujaona sehemu ya Theme kwenye app yako ya Instagram basi hakikisha una update app yako kupitia soko la Play Store au App Store. I hope umeweza kuwasha muonekano wa giza au dark mode kwenye app ya Instagram.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use