Hivi karibuni Instagram imekuwa ikijikita zaidi kwenye maboresho ya sehemu yake ya Stories na baada ya majaribio ya muda mrefu hapo jana instagram imeanza kuleta sehemu mpya ya Focus kwenye App zake za Android na iOS.
Kama tulivyosema awali kwenye makala ya kuhusu ujio wa sehemu hii, sehemu hii inakusaidia kuweza kuchukua picha ya sura yako vizuri na huku kwa nyuma kukiwa hakuonekani vizuri, yaani kunakuwa na ukungu flani au kwa kitaalam (blur). Sasa sehemu hiyo mpya ya Focus kwenye Instagram itakusaidia kuweza kupiga picha za aina hiyo, ambazo zitakuwa zina angalia zaidi sura yako kuliko sehemu nyingine za mazingira ya mahali unapo piga picha.
Kama unavyo ona kwenye picha hapo juu sehemu hiyo ya Focus imeng’arisha zaidi sura za watu kuliko maeneo mengine kwenye picha hiyo. Sehemu hii mpya ya Focus imesha anza kupatikana rasmi na unaweza kuipata kwenye sehemu ya kamera kupitia programu yako ya Instagram, kumbuka hiyo ni mara baada ya ku-update programu hiyo.
Hakikisha una angalia update za App ya Instagram kupitia soko lako la Play Store kama unatumia Android na App Store kama unatumia iOS ili kupata sehemu hiyo mpya.
Ahsante kwa kutupatia ujuzi ,maujanja n.k
Tatizo moja kwanini App yenu siku hizi inavikwazo inagoma kusakinisha kabisa
Mbona app iko sawa, unaweza kutujuza ni simu ya aina gani unatumia..?