Instagram imetangaza kufanya maboresho ya application hiyo katika sehemu ya “Feed”, maboresho hayo yamepanga kuondoa mfumo uliopo sasa ambao unaonyesha kila picha ya mtu unae mfollow hii inasababisha mtu kupitwa na matukio mengine ya watu wa muhimu.
Mabadiliko hayo ya sasa yatakua yanafanana na yale yaliopo kwenye Facebook ambapo utaweza kuona picha za watu kutokana na watu au picha uliyo like, Instagram iliandika kwenye blog yake kuwa “picha na video sasa zitakua zikionekana kwa mfumo wa “likehood” ama mfumo wa kuona picha au video za watu kutokana na like na comment”.
Instagram iliendelea kuandika kuwa asilimia 70% ya watumiaji wake wanakusa kuona picha na video muhimu kutokana na kuscroll kwa muda mrefu kutokana na kutumia mfumo wao wa zamani ujulikanao kama “Chronological Order”, mfumo huu wa zamani ulikua ili kuona picha za watu inakubidi kutembele ukurasa mzima ili kuona picha za watu unao wafuata au kuwa “follow”.
Sasa hivi Instagram itakuwa ikionyesha picha za watu ambao uko nao karibu tu na sio picha za watu wote ulio wafuata au kuwa follow. Instagram imesema kuwa mabadiliko hayo yatawafikia watu wote kuanzia mwezi ujao.