Mtandao wa instagram bado unaendelea kuwekewa maboresho mapya kila siku, siku za karibuni Instagram ilileta sehemu mpya ya Close Friend, sehemu ambayo inakuruhusu kutengeneza list ya watu unao wafahamu tu na kushare nao picha zako za kwenye sehemu ya Stories.
Sasa baada ya kuleta maboresho hayo siku ya leo Instagram imetangaza kuleta maboresho mengine kupitia sehemu ya DM. Kama wewe ni mtumiaji wa sehemu hiyo lazima utakuwa umeona sehemu mpya kwenye sehemu ya kuandikia ujumbe, sehemu hiyo iliyochorwa MIC itakupa uwezo wa kurekodi meseji za sauti kama ilivyo kwenye Voice Note ya WhatsApp.
Sehemu hii mpya itakuruhusu kurekodi meseji za sauti za hadi dakika moja, ili kurekodi sauti shikilia kitufe cha MIC huku unaongea pale utakapo maliza achia kitufe hicho na meseji yako itatumwa moja kwa moja. Kama utakuwa unataka kufuta utaweza kufanya hivyo wakati unarekodi kwani utaona sehemu ya kufuta iliyoko upande wa kushoto wakati unarekodi.
Kwa mujibu wa Instagram meseji hizo za sauti hazito futika baada ya muda hivyo pengine ni muhimu kuwa makini jinsi unavyo tumia sehemu hii hasa kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine hawajui kazi za mitandao ya kijamii. Anyway sehemu hii tayari iko kwenye programu za Instagram za iOS na Android hivyo unaweza kuiona sehemu hii pale unapotaka kum-DM mtu au pale unapofungua sehemu ya DM.